KISWAHILI KIDATO CHA TATU MADA YA 1: NGELI ZA MANENO

 NGELI ZA MANENO
  FORM THREE KISWAHILI STUDY NOTES TOPIC 1: NGELI ZA MANENO

 

Kuzielewa Ngeli
Upatanishi wa Kisarufi katika Sentensi
Ngeli ni vikundi vya majina ya Kiswahili. Ngeli za nomino ni utaratibu unaotumika kuweka nomino katika matabaka au makundi yanayofanana.
Mfano:
 1. Maji yakimwagika hayazoleki
 2. Mayai yaliyooza yananuka sana
 3. Yai lililooza linanuka sana
 4. Maji liliomwagika halizoleki
Katika mifano hii tunaona kwamba sentensi a, b na c ziko sahihi wakati sentensi d sio sahihi, hii ni kwa sababu imekiuka upatanisho wa kisarufi. Kwa maana hiyo sentensi ‘a’ ipo katika ngeli ya YA-YA na senthensi b na c zipo katika ngeli ya LI-YA. Sentesi d sio sahihi kwa sababu nomino maji haina wingi, kwa hiyo haiwezi kuingia katika ngeli ya LI-YA. Kwa msingi huu ngeli za nomino huzingatia sana upatanisho wa kisarufi.
Jedwali lifuatalo huonesha ngeli za nomino kwa misingi ya upatanisho wa kisarufi.
 

NGELI
 

UFAFANUZI
 

MIFANO
 

A-WA
 

Ngeli hii inahusisha majina ya viumbe hai kama vile wanyama, watu, wadudu, ndege n.k
 

Sungura mjanja ameumia Sungura wajanja wameumia Mkuu anawasili
 

LI-YA
 

Majina yenye kiambaisha awali li- katika umoja na ya- katika wingi huingia katika ngeli hii
 

Jambia la babu limepotea Majambia ya babu yamepatikana
 

KI-VI
 

Ni ngeli ya majina ya vitu visivyo hai, yanayoanza kwa KI- au CH- (umoja); na VI- au VY- (wingi). Pia ngeli hii hujumuisha majina ya vitu vingine katika hali ya udogo k.v, kijito, kilima
 

Chakula kimekwisha Vyakula vimekwisha Kijito kimekauka Vijito vimekauka
 

U-I
 

Huwakilisha majina ya vitu visivyo hai, yaanzayo kwa sauti M- (umoja) na MI (wingi). Pia majina ya baadhi ya viungo vya mwili huingia humu, kewa mfano mkono, mguu, mkia n.k
 

Mlima umeporomoka Milima imeporomoka Mkono umevunjika Mikono imevunjika Mto huu una mamba wengi Mito hii ina mamba wengi
 

U-ZI
 

Hurejelea majina ambayo huanza kwa U- (umoja) na huchukua ZI- kama kiambishi kiwakilishi cha ngeli katika wingi. Majina yenye silabi tatu au zaidi hubadilishwa kwa wingi kwa kutoa sauti /u/’ k.v ukuta-kuta. Majina ya silabi mbili huongezewa /ny/ katika wingi. k.v ufa – nyufa
 

Ukuta umebomoka Kuta zimebomoka Wimbo huu unavutia Nyimbo hizi zinavutia Ufa umeonekana Nyufa zimeonekana
 

I-ZI
 

Hutumiwa kwa majina yasiyobadilika kwa umoja wala kwa wingi lakini huchukua viambishi viwakilishi tofauti: I- (umoja) na ZI- (Wingi).
 

Nyumba imejengwa Nyumba zimejengwa Salam imefika Salam zimefika
 

U-YA
 

Ngeli hii inajumuisha nomino ambazo zina kiambishi awali u- katika umoja na ma- katika wingi.
 

Ukuu umekuponza Makuu yamekuponza Unyoya unapepea Manyoya yanapepea
 

KU
 

Majina yanayotokana na vitenzi yanayoanza na ku- (vitenzi-jina)
 

Kusoma kwako kumekusaidia Kuchelewa kumemponza
 

PA/MU/KU-
 

Huonesha mahali
 

Amekaa pale palipo na wadudu wengi Amelala mule mulimojaa siafu. Amepita kule mbali
Baadhi ya matumizi ya ngeli ni pamoja na haya yafuatayo:
 • Hutumika kupanga majina ya lugha katika makundi yaliyoshikamana na kutofungamana kutokana na kigezo muhimu.
 • Hutumika kutambulisha maumbo ya umoja na wingi katika majina na vivumishi.
 • Hutumika katika upatanishi wa kisarufi katika sentensi.
 • Hutumika katika kuonyesha uhusiano uliopo baina ya lugha za Kiswahili na lugha zingine.
Habari zenye Upatanishi wa Kisarufi
Baadhi ya matumizi ya ngeli ni pamoja na haya yafuatayo:
 • Hutumika kupanga majina ya lugha katika makundi yaliyoshikamana na kutofungamana kutokana na kigezo muhimu.
 • Hutumika kutambulisha maumbo ya umoja na wingi katika majina na vivumishi.
 • Hutumika katika upatanishi wa kisarufi katika sentensi.
 • Hutumika katika kuonyesha uhusiano uliopo baina ya lugha za Kiswahili na lugha zingine.
USIACHE KUSHARE HII POSTI NA NDUGU NA JAMAA KWA NJIA YOYOTE ILE

Leave a comment