Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Kwa ufasaa

Posted on

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Kwa ufasaa

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Kwa ufasaa


In English read here: How to Write an Application Letter
Barua ya maombi ya kazi huandikwa kwa malengo ya kuomba kazi. Kujifunza namna sahihi ya uandishi wa barua ya maombi ya kazi si kwamba utakusaidia katika kujibu maswali pekee, bali ujuzi huu utakufanya upate kazi halisi wakati utakapo hitaji kufanya hivyo.

MUUNDO WA BARUA YA MAOMBI YA KAZI

i.             Anuani ya mwandishi. Yaani anuani yako wewe unayeandika barua hiyo.
ii.            Tarehe.
iii.           Anuani ya anayeandikiwa.
iv.          Salamu.
v.           Kichwa cha habari.
vi.          Kiini cha barua. Hii ni roho ya barua yako, ukikosea mahali hapa, kama unajibu swali katika mtihani, utapoteza alama. Na kama unaomba kazi halisi, utaikosa. Kiini kina aya nne:
      Katika aya ya kwanza, eleza kazi unayoomba na mahali ulipoona tangazo la kazi hiyo. Ni katika sehemu hii unaweza kutaja umri wako.

      Katika aya ya pili, eleza ujuzi wako kwa ufupi. Usieleze sana. Barua hii haipaswi kuwa ndefu kupindukia.


      Aya ya tatu eleza kwa nini upewe kazi hii wewe na si mtu mwingine. Epuka kueleza shida zako binafsi ili upewe kazi. Maneno kama, ninaomba kazi hii ili niweze kumtibia mama yangu mgonjwa kitandani, hayana msaada.
      Aya ya nne eleza uko tayari kwa usahili siku gani?
vii.         Mwisho wa barua. Mwisho wa barua yako uwe na:
      Neno la kufungia. Wako mtiifuWako katika ujenzi wa taifa n.k
      Sahihi yako.
      Jina lako
Ni rahisi sana kuandika barua ya maombi ya kazi. Hebu tazama mfano wa barua hii:

TAZAMA MFANO WA BARUA YA KUOMBA KAZI

MTAA WA KIWALANI
S.L.P 3241,
DAR ES SALAAM.
24/4/2019.

MKUU WA SHULE,
SHULE YA SEKONDARIAZIKIWE,
S.L.P 45432,
DAR ES SALAAM.

Ndugu,

YAH: OMBI LA KAZI YA UALIMU

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 24. Najitokeza kuomba kazi ya ualimu katika shule yako kama ilivyotangazwa katika gazeti la Mwananchi siku ya Ijumaa ya tarehe, 21-4-2019.

Nimehitimu shahada yangu ya ualimu kwa masomo ya jiografia na Kiswahili mwaka 2015. Pia nimefanya kazi ya kufundisha kwa miezi saba katika shule ya wasichana Ktandaimba iliyoko mtwara. Mbali na hayo, nina uwezo mkubwa wa kutumia kompyuta.

Uzoefu wangu wa kazi na uwezo mkubwa wa kufundisha nilionao, unanishawishi niamini kuwa, ninafaa kufanya kazi katika shule yako.

Ninategemea majibu mazuri kutoka kwako. Pia, nipo tayari kwa usahili siku yoyote nitakayohitajika na nimeambatanisha nakala ya vyeti vyangu.

Wako mtiifu,

Sahihi

Ponda mari .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *