KISWAHILI KIDATO CHA NNE MADA YA KWANZA: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI

KISWAHILI KIDATO CHA NNE MADA YA KWANZA: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI

UNAWEZA JIPATIA NOTES ZETU KWA KUCHANGIA KIASI KIDOGO KABISA:PIGA SIMU: 07872327719

 

ALSO READ;

 1. O’ Level Study Notes All Subjects
 2. A’ Level Study Notes All Subjects
 3. Pats Papers

Uundaji wa Maneno

Lugha hukua na kubadilika kila wakati kulingana na maendeleo ya jamii. Kigezo kimojawapo cha kukua na kubadilika kwa lugha ni kuongezeka kwa msamiati. Ili msamiati uongezeke katika lugha sharti maneno mapya yaundwe.

Njia za Uundaji Maneno

Uundaji wa Msamiati hutokea kwa njia mbalimbali zifuatazo:
 1. Kubadili mpangilio wa herufi.
 2. Kuambatanisha maneno.
 3. Kutohoa maneno ya lugha nyingine.
 4. Uambishaji wa maneno.
 5. Kufanikisha sauti, umbo, mlio na sura.

Kuunda msamiati kwa kubadili mpangilio wa herufi

Neno hujengwa kwa vitamkwa au herufi. Neno jipya lenye maana tofauti huweza kuundwa kwa kubadili mpangilio wa neno lingine
Mfano
 • Neno lima, lina herufi l, i, m, a, herufi hizi huweza kujenga maneno kama mali, kumi,imla, mila.
 • Neno tua lina herufi t, u, a, herufi hizi zina weza kujenga maneno kama:- tatu, tua, viatu, tatua.

Njia ya kuambatanisha maneno

Kuna njia tatu za kuambatanisha meneno
Njia ya kurudufisha au kukariri neno
Mfano;  barabara, sawasawa, polepole, katikati, vilevile.
Njia ya uundaji wa Msamiati kwa kuunganisha maneno mawili tofauti
Nomino na Nomino
 • Punda + mlia unapata Pundamilia
 • Bibi + Shamba unapata Bibishamba
 • Afisa + Elimu unapata Afisaelimu
 • Mwana + Siasa unapata Mwanasiasa
 • Bata + maji unapata Batamaji
Kuunganisha kitenzi na Nomino/Jina
 • Changa + moto changamoto
 • Chemsha + bongo chemshabongo
 • Piga + mbizi pigambizi
 • Zima + moto zimamoto
Kuunganisha maneno mawili na kudondosha baadhi ya herufi
Mfano
 • Baraza la Kiswahili Tanzania BAKITA
 • Mzaliwa wa mahali Fulani MZAWA
 • Chama cha Mapinduzi CCM
 • Nyamamfu NYAMAFU

Kutohoa maneno kutoka lugha nyingine

Kila lugha na tabia ya kuchukua maneno lugha nyingine ili kukidhi mahitaji ya Msamiati. Maneno kutoka lugha nyingine yanapoteuliwa hubadilishwa kimatamshiili ya fuate kanuniza Kiswahili.
Maneno yanayotoholewa kutoka lugha nyingine husanifishwa na asasi za lugha ya Kiswahili ndipo ya ruhusiwe kutumiwa rasmi.
Mfano
Neno la Kiswahili
Lugha ya Mwanzo
Neno Lililotoholewa
Kijerumani
Schule
Salama
Kiarabu
Salaam
Duka
Kihindi
Dukan
Karoti
Kiingereza
Carrot
Shati
Kiingereza
Shirt
Picha
Kiingereza
Picture
Papai
Kihispania
Papaya
Meza
Kireno
Mezi
Shukrani
Kiarabu
Shukran
Ngeli
Kihaya
Engeli
Ikulu
Kinyamwezi
Ikulu
Ng’atuka
Kizanaki
Ng’atuka
Ndafu
Kichaga
Ndafu
Namba

Kuunda maneno kwa njia ya uambishaji wa maneno

Hii ni njia ya kubandika viambishi awali na tamati kwe nyekiini. Ujenzi wa maneno hutokana na mzizi mmoja kuonesha maana tofauti ingawa maana zina husiana.
Mfano mzizi: -lim-.Tukipachika viambishi awali na tamati tunapata maneno kama lima, analima, walilima, kilimo, limiana,halitalimwa na ukulima.
Kufananisha sauti, sura au tabia
Example 4
Mfano
 • Kengele – utokana na sauti ya kengele inapo pigwa
 • Pikipiki – hutokana na muungurumo wa pikipiki
 • Ndizi mkono wa tembo – Ndizi inayo fananishwa na mkono wa mnyama tembo
 • Chubwi – Jiwe au chura atumbukiapo katika kina cha maji.

Mazingira yanayoelezea Kuhitaji Maneno Mapya

Mabadiliko mengi yanatokea kila siku katika nyanja mbalimbali za kimaisha-mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa, kisayansi na kiteknolojia. Katika mazingira kama haya, watu watahitaji kuwasiliana, lugha itahitaji kuunda maneno ili kuwasilisha dhana mpya zilizoibuka. Kwa mfano, maneno kama vile nywila, kisakuzi, udukuzi, puku, talakirishi n.k yameundwa ili kuwasilisha dhana za kiteknoljia kwa Kiswahili.

Undaji wa Maneno katika Miktadha mbalimbali

Mabadiliko ya kimaendeleo yanafanya lugha ihitaji maneno ya kuyafikisha na kutumiwa na jamii. Ili kukidhi mahitaji hayo, maneno mapya yanazuka. Maneno hayo yanaweza kuwa katika fani mbalimbali, kama vile sayansi na teknolojia, siasa, utamaduni na uchumi kulingana na mkondo wa maendeleo. Mfano wa msamiati ni kama vile fedha, ushuru, kompyuta, ukoloni, hospitali, suruali n.k

 

JE UNAMILIKI SHULE AU BIASHARA NA UNGEPENDA IWAFIKIE WALIO WENGI?BASI TUNAKUPA FURSA YA KUJITANGAZA NASI KWA BEI NAFUU KABISA BOFYA HAPA KUJUA

 

SHARE THIS POST WITH FRIENDS

Leave a comment