KISWAHILI KIDATO CHA TANO:MATUMIZI YA SARUFI

MATUMIZI YA SARUFI

 

MATUMIZI YA SARUFI

USIBAKI NYUMA>PATA NOTES ZETU KWA HARAKA:INSTALL APP YETU-BOFYA HAPA

 

UNAWEZA JIPATIA NOTES ZETU KWA KUCHANGIA KIASI KIDOGO KABISA:PIGA SIMU:0787237719

 

FOR MORE NOTES,BOOKS,SCHEMES OF WORKS,PAST PAPERS AND ANALYSIS CLICK HERE

NADHARIA ZA SARUFI

Dhana ya sarufi ya lugha imefafanuliwa na wataalamu mbalimbali wa sarufi.

Mtaalamu  James Salehe Mdee (1999) sarufi ya Kiswahili sekondari na  vyuo  anafafanua maana ya sarufi  kuwa ni mfumo wa kanuni za lugha zinazomwezesha  mzungumzaji kutunga sentensi sahihi na zenye kukubaliwa na wazawa wa lugha. Kanuni hizi hujitokeza katika lugha ya mzawa wa lugha inayohusika ambaye anaifahamu barabara lugha yake. Sarufi inajumuisha mfumo wa sauti maumbo ya maneno muundo na maana.

Mtaalamu Mbundo Msokile (1992) na khamisi (1978) wanasema sarufi ni mfumo wa taratibu na kanuni zinazotawala matumizi sahihi ya matamshi, maumbo ya maneno, miundo ya tungo na maanda ya miundo ya lugha. Ni mfumo wa taratibu zinazomwezesha mzungumzaji wa lugha kutoa tungo sahihi na pia inamwezesha mtu yeyote anayezungumza kuelewa tungo zinazotolewa na mtu mwingine anayetuma lugha hiyo hiyo.

F. Nkwera (1978) anasema sarufi ni utaratibu wa kanuni zinazomwezesha mzawa au mtumiaji yeyote wa lugha kuelewa tungo zinazotolewa na mtu mwengine anayetunza lugha hiyo hiyo. Kufafanua nakuzielewa kwa undani tungo mbalimbali zitumikazo katika lugha hiyo pamoja na kutoa tungo sahihi na zinazoeleweka

HITIMISHO

Kwa ujumla maana zote  zilizotolewa na wataalamu wote ni maana sahihi za sarufi ila tunaweza kuhitimisha  kwa sarufi ni kanuni, sheria au taratibu zinazotawala lugha  katika viwango yote vya uchambuzi wa lugha yaani kiwango cha sarufi matamshi (fonolojia) sarufi maumbo (mofolojia) sarufi miundo (sintaksia) na sarufi maana (semantiki)

AINA ZA SARUFI

Ujumla sarufi inaweza ikagawanywa katika aina kuu zifuatazo

SARUFI  MATAMSHI (UMBO SAUTI)

Sauti katika lugha yaani jinsi ambavyo vitamkwa au sauti za lugha zinavyoungana ili kujenga maneno yanayokubalika katika lugha husika.

N.B: Sarufi matamshi hujishughulisha na uchambuzi wa sauti zilizomo katika lugha. Namna zinavyotamkwa, mahali zinapotamkwa na namna sauti hizo zinavyopangwa; ili kujenga maneno ya lugha Fulani.

Lugha mbili tofauti zinawezakuwa na sauti zinazofanana lakini zikatofautiana katika utaratibu wa kuzipanga sauti hizo.  Kila lugha ina utaratibu wake wa mpangilio wa sauti ili kujenga ama mofimu, silabi au maneno. Sauti zitumikazo katika lugha zinaweza kugawanywa katika makundi mawili

i.       Irabu, mfano a, e, i, o, u

ii.      Kansonati, mfano k, g, ch, i, d

FONIMU

Fonimu ni kipashio kidogo kabisa cha kifonilojia ni kitamkwa cha msingi cha kifonolojia kinacho badili maana ya neno

        MATUMIZI YA SARUFI

K, P, B  ni  fonimu kwani ndio zinafanya maneno hayo kutofautiana kimaana.

T na g ni fonimu zinazofanya maneno haya kutofautiana kimaana.

Irabu na konsonanti zinapotumika katika luga huitwa alfabeti.

Irabu ni sauti za lugha ambazo hutamkwa  bila kuwepo kwa kizuizi chochote kwenye mkondo wa  hewa utokao mapafuni kwenda nje kupitia chemba ya kinywa na pua..

SIFA ZA IRABU

1.      Irabu hutolewa kwa mrindimo wa ujenzi sauti

2.      Irabu zinapotamkwa midomo ya mtamkaji huviringwa na kutandazwa

3.      Utamkaji wa sauti hizi utegemea mkao wa ulimi katika chemba ya kinywa.

KONSONANTI

Ni sauti ambazo hutamkwa kwa kuzuia mkondo wa hewa katika sehemu mbalimbali kinywani hasa kwa kutumia ulimi.

i. Konsonanti ghuna: ni zile ambazo hutamkwa zikiwa na mrindimo mkubwa wa nyuzi sauti

ii. Konsonanti zisizosighuna(sighuna): ni zile ambazo hutamkwa zikiwa na mrindimo mdogo wa sauti

Katika Kiswahili sanifu, kuna konsonanti 23 na viyeyusho viwili hizo ni b, ch, d, dh, f, g gh, j, k, l,  m, n, h, ny, ng, p, r, s, sh, t, th, v, z.

Na viyeyusha viwili ambavyo ni : 

SILABI

Ni kitamkwa au sehemu ya neno ambayo hutamkwa mara moja na kwa pamoja kama sehemu ya fungu moja la sauti.

Silabi zinagawanyika katika makundi mawili

i.    Silabi funge

ii.  Silabi humo

i. SILABI FUNGE

Ni silabi zinazoishia na konsonanti

ii. SILABI HURU

Ni kitamkwa katika lugha (sauti katika luhga)

ALOFONI

Ni  vitamkwa tofauti yaani sauti zinabadili maana ya neno. Mfano

  MATUMIZI YA SARUFI

Bh na b ni alafoni zinazobadili maana ya neno

2.      SARUFI MAUMBO ( mofolojia)

Sarufi maumbo hujishughulisha na namna maneno ya aina mbalimbali yanavyoundwa katika lugha. Maneno katika lugha hujengwa kwa kuunganisha vipengele vidogo vya maneno ambavyo hubeba dhana mbalimbali kama vile nafsi,wakati,wingi,umoja, uyakinishi na kauli  mbalimbali n.k

Vipande  hivi vidogo vya maneno vijengavyo neno hufahamika kama mofimu, katika kila lugha kuna utaratibu wake  wa kuzipanga mofimu ili kujenga  maneno yenye  maana  katika lugha husika. Kwa kawaida mofimu hupangwa  kwa kufuata  utaratibu maalumu utarabu huo hujengwa  kama  utaratibu wa mpangilio kwa kufuata kanuni na huo utaratibu wa mpangilio wa  mofimu usipofuata  maumbo ya maneno   yasiyokuwa na maana yaani  yaliyokataliwa  na wazawa wa lugha husika. Utaratibu wa kuzipanga mofimu ili kuzalisha maneno yenye  maana katika  lugha husika hutuzalia kanuni maumbo kwa mfano katika lugha ya Kiswahili mofimu za umoja na wingi katika nomino huwekwa mwanzoni katika utaratibu huu haukubaliki katika  luhga ya kiingereza, katika lugha ya kiingereza mofimu za  umoja  na wingi huwekwa mwishoni mwa nomino. Mfano

Boy – boys

Girl – girls

Idea – ideas

N:B Kwa  ujumla sarufi maumbo (mofolojia) hujishughulisha na jinsi ambavyo mofimu mbalimbali zinavyoungana ili kujenga maneno yatumikayo katika lugha.  kipashio cha msingi katika mofolojia ya lugha ni mofimu.

3.      SARUFI MIZINGO/UMBO TUNGO (Miundo maneno / sintaksia)
uchunguzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi na  uhusiano wa maneno hayo  sintaksia huchunguza sheria au  kanuni zinazofuatwa katika  kuyapanga maneno ya lugha yaani mpangilio wa neno moja baada ya jingine kwa namna ambayo itayafanya maneno hayo yalete maana inayokubalika katika lugha inayohusika wakati mwingine mpangilio wa maneno unaweza ukawa sahihi yaani ulizounda utaratibu lakini ukazalisha tungo zisizo kuwa na maana hiyo zitakuza  mpangilio wa maneno wenye kuleta maana.

N:B  Katika  lugha  ya Kiswahili kanuni kubwa ya  kisintaksiani ni ile inayosema, kila sentensi iliyo sahihi na yenye kukubalika kwa  wazao wa lugha ya Kiswahili sharti iwe na muundo wakiima na kiarifu au kikundi nomino na kikundi kitenzi.

4.      SARUFI MAANA  (UMBO MAANA SEMANTIKI)

Tawi hili la sarufi huchunguza maana inayoonekana wazi na maana iliyofichika  huchunguza  muundo wa  tungo ili kupata maana iliyofichika. Katika lugha kila neno tungo huwa na maana yake. Kwa mfano, mtoto amelalia uji. Neno amelalia kama  lilivyotumika, Katika sentensi hii  halina maana moja na  hivyo kuifanya sentensi hiyo kuwa na maana zaidi ya moja,  mara nyingi  maana ya neno hutegemea matumizi ya neno katika  muktadha Fulani.

N.B.: Lugha inaweza ikafanya kazi sawasawa ambazo taratibu na kanuni za lugha husika zimefutwa.  Taratibu  hizo ni  zile  zinazohusu matamshi, maumbo,  muundo na  maana. Taratibu hizi ndizo humwezesha mzawa au  mtumiaji  yeyote wa lugha kutoa tungo sahihi na  zinazoeleweka  kwa matumizi  mengine ya lugha na  kuelewa tungo zinazokataliwa na watumiaji  wengine wanaotumia lugha hiyo hiyo.

VIPASHIO VYA LUGHA

Lugha hujengwa na vipashio mbalimbali ambavyo vinatabia ya kujengana yaani vipashio vidogo  huungana  kujenga vipashio vikubwa zaidi.lugha ina vipashio  vikuu vitano ambavyo ni

                        Mofimu – Neno – Kirai – Kishazi – Sentensi

Vipashio hivi wakati mwingine  hufahamika kama  tungo isipokuwa kipashio kidogo kwa vingine vyote katika lugha ni mofimu na kipashio  kikubwa kuliko vingine vyote ni sentensi vipashio vyote katika lugha vina muundo maalum unaoonesha jinsi vinavyojenga   vipashio vikubwa  kuliko vingine vyote ni sentensi, vipashio vyote katika lugha  vina muundo maalumu  unaonekana jinsi vinavyojengwa isipokuwa mofimu

MOFIMU

Mofimu ndio kipashio cha msingi kinachoshughulika katika mofolojia ya lugha kwa maana  mbalimbali za mofimu. Baadhi ya wataalamu  hujaza mofimu kwa kutumia  kigezo cha muundo wa  mofimu na wengine hufasili kwa kutumia kigezo cha kazi au dhima zinazobebwa na mofimu husika.

MAANA YA  MOFIMU

Mofimu ni sehemu ya neno au neno zima  lenye maana ya kisarufi au maana ya kileksika

AU

Mofimu  ni kipashio kidogo cha kimofolojia chenye kubeba maana iliyo ya kisarufi au ya kileksika

                       Mofimu hupangwa kwa kuzingatia utaratibu maalumu ili kujenga maneno yenye maana utaratibu huo hufahamika kama kanuni. Utaratibu wa upangaji wa mofimu ukikiukwa huzalisha maumbo yasiyokubalika katika lugha husika.

Mfano:          a – na – som – a neno hili linakubalika katika lugha kwa sababu mpangilio  wake wa mofimu umezingatia kanuni lakini mpangilio wake ungekuwa vinginevyo husingekuwa na maana

Mfano:           som – na – a –a tungezalisha umbo lisilokuwa na maana. Kila lugha inautaratibu wake wa kuzipanga mofimu

N.B                 Wakati mwingine mofimu huwa na maana sawa na neno, mofimu hizo huitwa mofimu huru au mofimu za kilekisika. Mofimu hizi husimama zenyewe bila kutegemea mofimu nyingine na huwa na maana kamili.

AINA ZA MOFIMU

Mofimu zinaweza zikagawanywa katika makundi mawili kwa misingi ya kikazi yaani mofimu za kileksika na mofimu zakisarufi. Pia zinaweza kugawanywa katika makundi mawili kwa msingi wa kimuundo na kupata mofimu huru na mofimu tegemezi.

1.      MOFIMU HURU (Mofimu  sabili/mofimu za kileksika)

Hizi ni mofimu ambazo husimama zenyewe zinaumbo dogo zaidi bila kupoteza maana. Aina hiyo ya mofimu hujitokeza katika aina mbali mbali za maneno;

 Mfano baba, Mama, kaka, na winnie ni nomino

-chafu, bovu, fupi, zuri na tamu ni vivumishi.

-Hata, lakini, kama, mpaka, au- viunganishi

-Arifu, tafiti, samehe- vitenzi

Mofimu zote huru huwa  na kazi ya kileksika

2.      MOFIMU TEGEMEZI

Hizi ni mofimu ambazo haziwezi kusimama ili kukamilisha dhana iliyokusudiwa. Mofimu tegemezi hujumuisha mofimu awali, mzizi, na mofimu tamati.Mpangilio wa

mofimu hizo au mfungamano wa mofimu hizo huunda neno. Mofimu hutumika katika kuunda maneno

N.B Mofimu tegemezi zinapofungana huunda neno tegemezi, mfano: a – na – som – a anasoma, nam – pend – a – nampenda

Mofimu huru huunda neno huru mfano, Baba, mama starehe, jaribu n.k Mfungamano wa mofimu huru na mofimu tegemezi hujenga neno changamano. Mfano; mw – ana – nchi

Mw – ana – anga

KUBAINISHA MOFIMU

Kubainisha mofimu ni kuligawa neno katika mofimu zinazolijenga neno na kueleza kazi za kila mofimu ubabaishaji huo wa mofimu hufuata hatua zifuatazo

1.  Kutambua aina ya neno – Yaani kama neno hilo ni tegemezi au neno changamano, Neno huru huundwa na mofimu huru na neno tegemezi huundwa na mofimu tegemezi na neno changamano huundwa na moja  huru na mengine tegemezi

                 N: B Neno huru huwa halivunjwi vunjwi kwani huundwa na mofimu huru

2.      Kulitenga neno na kulivunja vunja katika mofimu zinazojenga neno hilo yaani hujenga mofimu awali, mzizi na mofimu tamati.

N: B Mofimu awali, mzizi na mofimu tamati hupatikana katika maneno tegemezi na maneno changamano

3.      Kueleza kazi ya kila mofimu

Mfano: Bainisha mofimu katika maneno yafuatayo

Hatukupendi

Hili ni neno tegemezi

MATUMIZI YA SARUFI

ii.               1- Mofimu awali kianzishi, nafsi ya kwanza wingi

2 – Mofimu awali rejeshi kwa mtendwa

3 – Mofimu awali rejeshi kwa mtenda

4 – Mofimu mzizi

5 – Mofimu tamati kanushi

6. Asiyekujua

  i.   Hili ni neno tegemezi

MATUMIZI YA SARUFI

iii.   1. Mofimu awali nafsi ya tatu umoja

2. Mofimu awali kanushi  nafsi ya  tatu umoja wakati uliopo

3-Mofimu ya urejeshi kwa mtenda

4-Mofimu awali ya urejeshi kwa mtendwa

5-Mofimu mzizi

6. Mofimu tamati

C. Kikikitangulia

i.          Hili ni neno tegemezi

    MATUMIZI YA SARUFI

ii   1.    Mofimu awali nafsi ya tatu umoja

       2.   Mofimu awali kanushi ya nafsi ya tatu umoja wakati uliopo

       3    Mofimu ya urejeshi kwa mtenda.
4.   Mofimu mzizi
5.   Mofimu tamati

5.

7.

 d. Nimejikata

   i. Hili ni neno tegemezi

MATUMIZI YA SARUFI

ii 1 – Mofimu awali ya nafsi ya kwanza umoja

     2 – Mofimu awali inayoonesha hali timilifu

3        – Mofimu  awali ya urejeshi wa  kujitendea

4        -Mofimu mzizi

5        -Mofimu tamati

e. Sipendeki

          Hili ni neno tegemezi

        -Si- pend – ek –i
1      2      3    4

1.        – Si – mofimu awali kanushi nafsi ya  kwanza umoja wakati uliopo.
2.        – pend- mofimu mzizi
3.        -ek- mofimu tamati ya kutendeka
4.        -i- mofimu tamati ya ukanushi

DHIMA ZA MOFIMU

Mofimu huwa na dhima au kazi mbalimbali zinazotumika katika maneno.

 Kazi za mofimu ni kama  zifuatazo:-

1.      Kuongeza msamiati katika lugha au kubadili maneno kutoka kategoria moja kwenda kategoria nyingine.

Mfano: Nyumba – Nyumbani

            Soma – somo

            Soma – msomi

            Taifa – taifisha.

2.      Kuongeza maana ya ziada au kupanua  maana ya neno

Mfano: Taifa – Utaifa

3.      Kudokeza dhana ya umoja na wingi

Mfano: Mtu – watu

iii.               Ni majina yenye umbo la umoja lakini umbo la wingi hakuna

Mfano:    Umoja                      Wingi

                Ukuta                        Kuta

                U – Funguo               Funguo

                U-Kucha                   Kucha

                U-kope                      kope

iv.               Ni maneno ambayo  yana umbo dhahiri la wingi lakini umbo la umoja  halipo

Mfano:   Umoja                      Wingi

               Ukuta                         Kuta

               U- Funguo                 Funguo

               U-Kucha                    kucha

               U-Kope                      kope

v.                  Ni nomino ambazo zina umbo dhahiri la wingi lakini umbo la umoja halipo

Mfano:   Umoja                       Wingi

                 Boga                          Ma-boga

                 Jembe                        ma-jembe

                 Debe                          Ma-debe

                 Tako                          Ma-tako

                 Panga                         Ma-panga

iv.   Ni majina yanayokuwa na mofimu  ya wingi wala umoja

Mfano:                     Umoja                        Wingi

                                  Boga                          ma – maboga

                                  Debe                          ma – debe

                                  Tako                          Ma-tako

                                  Panga                         Ma-panga

v.      Ni majina yanayokuwa na mofimu ya wingi wala umoja

Mfano:                     Umoja                        Wingi

                                  Shule                         Shule

                                  Ng’ombe                   Ng’ombe

                                  Mbuzi                        Mbuzi

                                  Kuku                          Kuku

N.B:   Mofimu  kapa hujitokeza  katika kundi la pili (2) na kundi la tatu (3) ambapo katika kundi la pili (2)  katika umoja  majina yana mofimu (2).  Mofimu ya kwanza inaonesha umoja na mofu ya pili inaonesha mzizi wa neno.

 Katika wingi mofu ya  wingi ni kapa ambayo hufuatiwa na mofu ya pili inaonesha mzazi wa neno. Katika wingi mofu ya wingi ni kopa ambayo hufuatiwa na mofu mzizi na kuzifanya nomino hizo kuwa na mofu mbili. Mofu ya kwanza  ni kapa ambayo hudokeza wingi  na mofimu ya pili ni mzizi. Japokuwa mofu ya wingi ni kapa yaani haiandikwi wala kutamkwa   athari yake ipo.

DHIMA ZA MOFIMU
1.Kuonesha udogo wa kitu au ukubwa wa kitu

 Mfano: Kijiti-jiti

Kuondoa upatanisho wa kisarufi ambao hutawaliwa na nomino ya kiima na kitenzi.
Mfano: Kiti kimevunjika.
Utaratibu huu haufai.
Sheria hii haifai.

Kudokeza nafsi mbalimbali.
Mfano: ni….na….som….a-nafsi ya kwanza umoja.
Tu….na….som….a-nafsi ya pili umoja
U-na-som-a- nafsi ya pili wingi
A-na-som-a- nafsi ya tatu umoja
wa-na-som-a- nafsi ya tatu wingi.

4. Kudokea njeo/wakati
Mfano: Atakuja- Wakati ujao
Atakapokuja- Wakati uliopo timilifu.
Amekuja- Wakati uliopita timilifu.
Alikuja- Wakati uliopita.

5.Kudokeza hali mbalimbali katika tungo.
Mfano: Hucheza- Hali ya mazoea.
Akija- Hali ya masharti.
Angekuja

6.Kudokeza urejeshi kwa mtenda mtendwa mtendwa kujitenda au tendo kwa mtenda.
Mfano: Aliyenipiga- Inaturejesha kwa mtenda.
Aliyenipiga- Inaturejesha kwa mtenda.
Aliyesomea-Inaturejesha kwa mtendewa
Nimejikata- Inarejesha tendo kwa mtenda (kujitenda)

7.Kuonesha ukanushi.
Mfano: Hakuja
Sisomi

8. Mofimu hudokeza kauli mbalimbali
Mfano: Kauli ya kutendwa- Pigw-pig-w-a

Kauli ya kutendewa-pig-iw-a

Kauli ya kutendea-pig-i-a

Kauli ya kutenda-pig-a

Kauli ya kutendeana-pig-an-a

Kauli ya kutendeshwa-pig-ian-a

Kauli ya kufungamanisha-gandamana

Kauli ya kutendwa-choma-chomoa
-funga-fungua

Kauli ya kutendaka-fumba- fumbata
-ambaa-ambata

      4.   Kuonesha udogo wa kitu au ukubwa wa kitu

  Mfano: Kijiti – jiti

  1.       Kuondoa upatanisho wa kisarufi ambao hutawaliwa na  nomino ya kiima na kitenzi

Mfano: Kiti kimevunjika.

             Utaratibu huu haufai.

             Sheria hii haifai.

  1.       Kudokeza nafsi mbalimbali

Mfano:             ni ……na…. som ….a – nafsi ya kwanza umoja

                         Tu… na…som…a————-nafsi ya pili umoja

                         U-na-som-a ————– nafsi ya pili wingi

                         A-na-so-a——————- nafsi ya tatu umoja

                        wa – na—som—a———–nafsi ya tatu wingi

  1. Kudokeza njeo/wakati

   Mfano:       Atakuja – Wakati ujao

                       Atakapokuja – Wakati uliopo timilifu

                       Amekuja   – Wakati uliopita timilifu

                        Alikuja    – wakati uliopita

8.     Kudokeza hali mbalimbali katika tungo

 Mfano: Hucheza – hali ya mazoea

                Akija – Hali ya masharti

                Angekuja

9. Kudokeza urejeshi kwa mtenda mtendwa mtendwa jujitenda au tendo kwa mtenda

   Mfano: Aliyenipiga – Inaturejesha kwa mtenda

                 Aliyenipiga – Inaturejesha kwa mtendwa

                  Aliyesomea – inaturejesha kwa mtendewa

                  Nimejikata – inarejesha tendo kwa mtenda (kujitenda)

10. Kuonesha ukanushi

      Mfano: Hakuja

                  Sisomi

11. Mofimu hudokeza kauli mbalimbali

      Mfano: Kauli ya kutendwa – Pigwa – Pig- w-a

                   Kauli ya kutendewa    pig-iw –a

                   Kauli ya kutendea- pig –i – a

                   Kauli ya kutenda –Pig  –a

                   Kauli ya kutendeana – Pig – an –a

                   Kauli ya kutendeshwa – pig-ian –a

                   Kauli ya kufungamanisha – gandamana

                   Kauli ya kutendwa – choma   – chomoa

                                                     -Funga – fungua

                     Kauli ya kutendaka –   fumba – fumbata

                                                          Ambaa – ambata

ALOMOFU

Alomofu ni maumbo zaidi ya moja au maumbo tofauti ambayo huwakilisha mofimu moja kisanji ambayo hufanya kazi moja kisaruji alomaju hutokea mazingira maalum baadhi ya mazingira hutabirika mengine hayatabiriki kabisa. Alomofina kwa kawaida kubadili maana ya neno.

UTOKEAJI WA ALOMOFU

  1.       Mazingira ya kifonolojia (matamshi)

Kwa kutumia utawala au mazingira tunaweza kupata mofimu na alama yake kwa vitenzi vya lugha ya Kiswahili vinaponyumbuliwa huzalisha kauli mbalimbali, kauli hizo hudhihirika kutokana na kuwepo kwa mofimu mahususi zinazoonesha kauli husika.

Kauli ya kutendewa

Kauli hii inahusisha tendo ambalo hutendwa   na muhusika Fulani kwa niaba ya wahusika mwingine. Maumbo ambayo huonesha kauli hiyo ya kutendwa ni (-iw-) (-ew-) na (-liw-) na (-lew-). Mambo haya hufahamika kama alomofu na utokeaji wake hutegemea athari za kimatamshi za kitenzi husika

Mfano: Lima – Lim – iw –a

             Suka – suk – iw – a

            Cheza – chez – ew –a

            Paka –  pak – iw – a

            Soma – som – ew –a

            Kimbia – kimb – liw –a

            Tafiti – tafit – iw –a

            Zoa – zo – l-ew –a

            Chomoa – chomo – lew –a

Mofimu ya kauli ya kutendewa ina alomofu tano ambazo ni

(-iw-) hii hutokea ikiwa mzizi wa kitenzi unaishia na konsonanti na mzizi huo una irabu a,e,I,o,u.

  •         (ew-) hii hutokea ikiwa mzizi wa kitenzi unaishia na konsonanti na mzizi huo unairabu e au o
  •         (-liw-) hutokea ikiwa mzizi wakitenzi unaishia na irabu i, a , au u
  •         (-lew-) hutokea ikiwa mzizi wa kitenzi unaishia na irabu a au e
  •         (-w-) hutokea kama mzizi wa kitenzi unaishia na irabu- i -lakini kwa vitenzi vya kuchukua yaani visivyokuwa na asili ya kibantu.
  1.       Mazingira ya kileksika

Kwa kutumia mazingira ya kileksika alomofu zinaweza kutokea katika ngeli za majina kwa mfano katika ngeli ya kwanza na y apili yaani m/w inaweza kuona alomofu ageli ya kwanzakama ifuatavyo:-

NGELI II                        NGELI 1

Wa –tu                              M-tu

Wa-ke                               M-ke

Wa-nafunzi                      Mw-anafunzi

Wa-elevu                          Mw-elevu

 Wa-wezeshaji                 Mw-ezeshaji

Wa-imbaji                        Mw-imbaji

Wa-ongozaji                    Mw-ongozaji

Wa-uguzi                          Mu-uguzi

Wa-umbaji                       Mu-mbaji

Katika ngeli ya kwanza mofimu m –inaonesha umoja .katika ngeli hiyo ya kwanza ambayo kiwakilishi chake ni mofimu m- kuna maumbo matatu ambayo hufanya kazi ya kuonesha umoja katika ngeli- I- maumbo hayo ni;

Kwa hiyo ngeli ya I ina alomofu tatu alomofu ni (m-) (mw-) (-mu-)

  •         Alomofu (m-) hutokea inapofuatwa na konsonanti
  •         Alomofu (m-) hutokea inapofuata  na irabi a, e, i, o
  •         Alomofu, (mu-) hutokea inapofuatwa na irabu- w
  1.       Mazingira ya kisarufi

Kwa kutumia mazingira ya kisarufi tunaweza kupata mofimu na alomofu zake hasa katika mofimu njeo.  Mofimu rejea inawakilishwa na maumbo yafuatayo.

a-li – soma

a-me – soma

a-na-soma
a-     Ta- soma

Mofimu njeo inaolomofu nne alomofu hizo ni  (-li-) (-me-) (-na-) na (-ta-)

  •         Alomofu (-li-) na (-ta-)
  •         Alomofu (-me-) hutokea kuonesha wakati uliopita  timilifu
  •         Alomofu (-na-) hutokea kuonesha wakati uliopo
  •         Alomofu (-ta-) hutokea kuonesha wakati ujao.

N.B: ingwa alomofu ni maumbo yanayotofautiana hufanya kazi moja kisarufi. Maumbo hayo hutokea katika mazingira maalumu ambayo yanaweza yakatabirika au yasitabirike kabisa mazingira hayo yanaweza kuwa ya kifonolojia au mazingira ya kileksika na mazingira ya kisarufi.

VIAMBISHI

Baadhi ya watu huchanganya dhana ya viambishi na dhana ya mofimu. Lakini ukweli ni kwamba mofimu na viambishi ni dhana  mbili tofauti zenye mabwiano Fulani pia. Kwa  ujumla viambishi vyote ni mofimu   na mofimu zote ni viambishi

SWALI: VIAMBISHI NI NINI?

Viambishi  ni mofimu  zinazoandikwa kwenye mizizi wa neno ili kukamilisha muundo wa neno husika. Katika lugha ya Kiswahili viambishi vinaweza kuandikwa kabla ya mzizi wa neno na baada ya mzizi wa neno.

 kwa hiyo katika lugha ya kiswahili viambishi hutokea kabla ya mzizi wa neno na baada  ya mzizi wa neno

AINA ZA VIAMBISHI

Lugha  ya Kiswahili ina viambishi vya aina mbili

  1. VIAMBISHI AWALI/TANGULIZI

Hivi ni viambishi ambavyo hutokea mwanzoni mwa mzizi wa neno na huwa ni vya aina mbalimbali

           A.Viambishi idadi /ngeli

Viambishi hivi hupatikana mwanzoni mwa majina vivumishi kwa lengo la kuonesha idadi yaani wingi na umoja, Mfano :

M – cheshi     wa –zuri

M – tu            wa  – tu

Ki – ti              vi-ti

m- ti               mi  – ti

N:B Wakati mwingine katika majina na vivumishi  huweza kuandikwa, viambishi ambavyo hudokeza ukubwa  wa nomino  na  vivumishi. Hivyo  wakati mwingine  majina  na vivumishi huandikwa viambishi ambavyo hudondokea   udogo wa majina na vivumishi.

Mfano: ji – tu      ma – jitu

            Ju –mba     ma – jumba

            Ki – toto     vitoto

            Ki –vulana   vi – vulana

            Ki – zuri       vi – zuri

B. Viambishi awali vya ukanushi

Viambishi vya ukanushi kwa kawaida huwekwa mwanzoni mwa vitenzi ili kukanusha vitenzi husika.  Viambishi ambavyo huandikwa katika vitenzi vya lugha ya Kiswahili ili kuonesha ukanushi wa tendo ni viambishi,

“Si”   “ha” na “bu”

Kiambishi “ha” hutumika kukanzisha kitenzi kilichofanywa na nafsi ya kwanza wingi nafsi ya pili wingi na nafsi ya tatu katika umoja na wingi.  Katika nafsi ya pili hutumika alomofu “ku” ambayo hukanusha nafsi ya pili umoja

Mfano:   ni  – na — imba  —si —imbi

               U – na – imba – hu – imbi

              Tu  – na –imba — ha –tu — imbi

              m- na – imba – ha —  mu— imbi

              wa —na – imba — ha —wa –imbi

C. Viambishi vipatanishi / nafsi

Hivi ni viambishi ambavyo huwekwa kabla ya mzizi wa kitenzi na kubadilika kutegemeana na aina ya neno linalopatanishwa na kitenzi husika, kazi ya viambishi hivi ni kuonesha nafsi.
Mfano;

      Ni – nasoma     tunasoma

      A   – nasoma     m – mnasoma

      U- nasoma      wa – nasoma

  1.       Viambishi vya njeo /wakati

Kiambishi cha njeo ni kiambishi ambacho huwekwa katika kitenzi ili kuwakilisha muda ambapo tendo husika limetendeka. Mfano tendo kama limefanyika wakati uliopita huwakilishwa na kiambishi (-li-) katika uyakinishi na kiambishi (-ku) tendo hilo linapokanushwa

Ni- li—soma                     Si – ku – soma

U – li- soma                     hu – ku – soma

A – li- soma                     ha – ku-soma

Tu – li – soma                 hatu-ku-soma

M-li – soma                     ham-ku-soma

Wa – li- soma                     hawa-ku-soma

  1.       Viambishi vya hali

Hivi ni viambishi ambavyo huwekwa kabla ya mzizi ambavyo hutumika kuonesha muda au kipindi maalum ambao tendo, lilifanyika viambishi vya hali hueleza kama tendo linaendelea kufanyika kama hufanyika mara kwa mara kama limemalizika kufanyika

  1.      Hali ya kuendelea kwa tendo

Hali ya kuendelea kwa tendo huwakilishwa na kiambishi (-na-) ambacho huwekwa kabla ya mzizi wa kitenzi

Mfano     ni  – na – imba

                Tu – na-imba

                 U-na-imba

                 M-na-imba

                 A-na-imba

                 Wa-na-imba

  1.     Hali timilifu

Hali hii huwakilishwa na kiambishi”me” katika uyakinishi na kiambishi  “ja” katika ukanushi. Mfano:

Ni – na-soma           Si – ja- soma

Tu-me-soma            hatu-ja-soma

M-me-soma             ham-ja-soma

A-me-soma              ha-ja-soma

Wa-me-soma           hawa – ja-soma

  1.     Hali ya mazoea

Hali ya mazoea huwakilishwa na kiambishi (-hu-)

Mfano:     hu – soma

                 hu – imba

                 hu –cheza

                 hu – cheza

                 hu- lala

  1.     Hali ya masharti

Hali ya masharti huwakilishwa na viambishi (-ki-) (-nge-)

Mfano: kiambishi (-ki-) hudokeza uwezekano

Tu-     Ki-shinda – tukishinda tutafurahi

A-ki-ja – akija nitamwambia

Kiambishi (-nge-) hudokeza matumaini kidogo

                        A-nge-nilipa-Juma pesa yangu ningenunua gari.

Kiambishi (-ngali-) hudokeza kutokua na matumaini yeyote au kuwepo kwa matumaini kidogo kuliko yale yanayodokezwa na kiambishi (-nge-); mfano ningalijua kua nitafeli mtihani ningalisoma kwa bidii.

  1.        Viambishi vya mtenda

Hivi ni viambishi ambavyo hurejesha tendo kwa nomino ya mtenda, viambishi hivi hutegemea aina ya nomino inayorejeshewa

Mfano: ali – ye – piga

             Uli-o-vuna

             Vili-vyo-anguka

g.Viambishi vya urejeshi kwa mtendwa (yambwa)

    Hivi ni viambishi ambavyo hurejesha tendo kwa nomino ya mtendwa wa jambo

Mfano: ali – ye-pigwa

            Ali – o- vunjwa

            Vili – vyo – angushwa

h. Viambishi virejeshi kwa mtendewa  (kiambishi yambiwa)

Hivi ni viambishi ambavyo hurejesha tendo kwa nomino ya mtendwa jambo

Mfano: ali – ye-somewa

  1.      Viambishi vya urejeshi wa kujitendea

Hivi ni viambishi ambavyo hutokea kabla ya mzizi wa kitenzi na huwakilishwa na kiambishi (-ji-) ya kujitendea ambavyo hutumika katika umoja na wingi na pia katika uyakinishi na ukanushi

Mfano:            nili – ji-somea          siku – ji- somea

                        Nime- ji-kata             sija-ji-kata

                        Nina-ji-somea           si – ji-somei

                        Ana-ji-somea             ha-ji-somei

                        Una-ji-somea            ha-ji-somei

                        Tun-ji-somea            hatu-ji-somei

                        Tuta-ji-somea           hatuta-ji-somea

                        Mta-ji-somea           hamta-ji-somea

                        Wali-ji-somea         hawaku-ji-somea

  1.       VIAMBISHI KATI

Viambishi kati ni viambishi ambavyo hupachikwa ndani ya mzizi wa neno na hivyo kuukata mzizi katika sehemu kuu mbili (2)

N.B; Viambishi kati huwepo katika lugha ya Kiswahili kwa sababu maneno ya lugha ya Kiswahili kwa tabia yake hawaruhusu upachikaji wa viambishi kati ya mzizi, viambishi hivi hutokea katika lugha nyingine mfano kiebrania.

  1.       VIAMBISHI TAMATI

Hivi ni viambishi ambavyo huiweka baada ya mzizi wa neno. Navyo ni vya aina kuu mbili (2)

(a)  Viambishi tamati maana

(b)  Viambishi  tamati vijenzi

  1.       Viambishi tamati maana

Viambishi tamati maana ni viambishi ambavyo hukamilisha maana ya neno. Viambishi hivi huwa haviadhiri maana ya awali ya neno yaani havijengi dhana mpya katika neno

Mfano: a-na-som-a

             Tend –a

              Kata –a

              Kat –a

  1.       Viambishi tamati vijenzi

Hivi ni viambishi ambavyo hujitokeza mwishoni mwa mzizi wa neno ili kujenga dhana mpya

Mfano: piga – pig -o

               Mcheza – Mcheza-ji

               Soma – som -a

Viambishi tamati hufanya kazi mbalimbali kama vile kudokeza kauli mbalimbali za vitenzi

i. Kauli ya kutenda

 Hii ni kauli ambayo hueleza jambo lililotendwa na mtenda. Viambishi ambavyo hubainisha kauli ya kutenda ni viambishi tamati maana ambavyo huwa ni vimalizio vya mzizi wa kitenzi

Mfano gand – a

            Pig – a

Som –a

ii.Kauli ya kutendwa

Kauli hii hueleza kuwa mtu, watu au vitu Fulani vimetendwa jambo Fulani, Alomofu ambazo huwakilisha kauli ya kutendwa ni (-wa) (-liw) (-lew-)

Mfano: pig – w-a

            Sem – w-a

            Chom- w-a

             O – lew – a

            Vu – liw – a

           Ambi – w-a

iii.Kauli ya kutendewa

   Kauli hii huonesha kuwa mtu Fulani ametenda kwa niaba ya mtu mwingine, Alomofu ambazo hutumiwa kuonesha kauli ya kutendewa ni (-iw-), (ew-) (-liw-) (-lew-)

Mfano: lim – iw-a

             Chez-ew-a

             Som-ew-a

              Kimbi-liw-a

              Zo-lew-a

              Va-liw-a

              Chomo-lew-a

IV. Kauli ya kutendea

 Kauli hii huonesha kuwa tendo limefanyika kwa manufaa, kwa niaba au kwa faida ya mtu mwingine alomofu za kauli ya kutendea ni (i) (-e-) (-li-) (-)

Mfano: pig – i-a

             Lal – i-a

             Ruk-i-a

             Chez-e-a

             Zo-le-a

              o-le-a

V. Kauli ya kutendesha

  Kauli hii huonesha wababaishaji ambao huwezakuwa na mhusika au wahusika  Fulani  wanaosababisha  kufanyika kwa tendo la mhusika   na wahusika wengine. Kauli hii huonesha   mtu fulani wanavyosababisha  kufanyika  kwa tendo  kwa mhusika  na wahusika wengine. Kauli hii huonesha mtu Fulani anamsababishia mtu mwingine kufanya jambo  Fulani  za  utendaji (-ish) (esh-) (-lish)  (-lesh-) (sh) na (-z)

Mfano :  imb – ish –a

               Kimbi – z –a

               Tembe – z-a

               Pit – ish –a

               ru – sh –a

  VI. kauli ya kutendesha (usababishaji)

   Ni kauli ya wasababishi ambao huwezakuwa ama mhusika au wahusika Fulani wanaosababisha kufanyika kwa tendo kwa mhusika au wahusika wengine. Kauli hii huonesha   mtu fulani ana msababisha mtu mwingine kufanya jambo Fulani.

               Og – esh –a

               Zo-lesh-a

              Ka-lish – a

              Va-lish-a

              Shon-esh-a

              Som-esh-a

             Chem-sh -a

Vii. Kauli ya kutendana

 Kauli hii huonesha  wahusika Fulani kuhusika na tendo Fulani ambapo mhusika wa kwanza anamtenda mhusika wa pili, lakini  pia mhusika wa pili ana mtendea mhusika  wa kwanza katika jambo   hilo hilo.

 Adhari ya tendo linalofanyika huwa kwa pande zote mbili yaani mtu wa kwanza na mtu wa pili. Kauli hii hudhihirishwa na kiambishi (-an-) ambacho hutokea baada ya mzizi wa kitenzi.

Mfano: pend – an-a

             Suk – an –a

             Sukum – an –a

             Sem – an – a

             Ruki – an –a

Viii. Kauli ya kutendeana

 Kauli hii huhusisha tendo linalofanywa na watu wawili ambapo mhusika wa kwanza anafanya tendo Fulani wka  mambo ya mhusika wa pili na muhusika wa pili anafanya tendo hilo  hilo kwa niaba ya muhusika wa kwanza. Kiambishi kinachodhihirisha kauli hii ni (-an-) ambayo hutokea kati ya kiambishi kinachofuata baada ya mzizi wa kitenzi na kiambishi tamati maana

Mfano:    suk – i – an –a

               Sem-e-an-a

               Som-e-an –a

               Zo-le-an-a

               Va-li-an-a

                O-le-an-a

ix. Kauli ya kutendana (kufungamana)

 Hili ni kauli ambayo hurejelea hali, ambapo watu au kitu hukaa pamoja kwa muda mrefu. Mofimu ya kauli hii katika lugha ya Kiswahili ni  (-am-) ambayo hujitokeza  katika vitenzi vichache

Ung – am-a

Ach – am –a

x. Kauli ya kutendwa

 Hi ni kauli ambayo huonesha kinyume cha tendo. Na kauli hii hudhihirishwa na kiambishi (-o) na (-u-)

Mfano: umb – u –a

             Teg – u – a

             Chom – o –a

             Kunj – u-a

             Pang – u –a

Xi Kauli ya kutendana (kishikanishi)

Hii ni kauli inayoonesha mshikamano yaani tendo la kufanya watu au vitu kushikana na mofimu inayodhihirisha kauli hi ni (-at-)

Mfano:Pak-at-a

             Kam-at-a

             Fumb – at – a

SHINA NA MZIZI

Mzizi /kiini ni sehemu ya neno inayobakia baada ya kuondoa aina zote za viambishi yaani viambishi vya awali vyote na viambishi tamati vyote.

Mzizi ni sehemu ya muhimu ambayo hubeba maana   ya msingi katika neno

AINA YA MZIZI

Kuna aina kuu mbili (2) za mzizi

  1.       Mzizi fungo/tegemezi

Huu ni mzizi ambao hauwezi kujitegemea yaani huwezikusimama peke yake kama neno na kuleta maana

Mfano: som — a

             Chom – a

              Pend   -a

(a)  (chom-), ( som) na (pend-) ni mzizi tegemezi ambayo haiwezi kusimama yenyewe bila kuleta maana

  1.       Mzizi huru/sahihi

Huu ni mzizi ambao unaweza kusimama peke yake kama neno na kuleta maana.

Mfano: Jembe

             Ng’ombe

             Winnie

              Marcus

              Abel

              Concepta

 

Shina ni nini?

Shina ni sehemu ya neno (mzizi asilimia waneno) ambayo hufungamanishwana irabu mwishoni isiyokuwa na maana maalum kisaruji

Mfano:                     Neno              shina

                                   Mtoto             toto

                                   Wanacheza   Cheza

AINA ZA MASHINA

  1.       Shina sahili /huru

Hili ni shina ambalo huundwa na mofimu moja tu ambayo pia huwa ni mzizi wa neno. Mfano ng’ombe, kuni, tafiti

  1.       Shina  changamano

Ni shina ambalo huundwa na mzizi pamoja na kiambisi mwishoni, Mfano cheza soma, na kimbia.

  1.       Shina ambatani/ ambatana

Hili ni shina ambalo linaundwa na mofimu mbili ambazo zote huwa ni mzizi

Mfano: mwana + nchi

            Pima + Maji

NB: Katika lugha ya Kiswahili wakati mwingine hulingana na mzizi na mofimu. Kulingana kwa dhana hizo hakuna maana kwamba dhana hizo ni sawa.

DHANA YA MOFU

 

Dhana ya mofu inafafanuliwa na wataalamu mbalimbali wa sarufi kama ifuatavyo;

Mtaalamu (Nick 1949) anafafanua mofu kuwa ni umbo la neno ambalo huwakilisha mofimu na ambalo hudhihirika kifonolojia na kiothografia.

Mofimu ambazo elementi dhahania, huwakilishwa na mofu ambazo hudhihirika kifanolojia zikiwa na sauti za kutamkwa, au kiothografia zikiwa ni alama za kuandikwa.

TUKI (1990) wanafafanua kuwa mofu ni kipashio cha kimofolojia kiwakilichasho mofimu

 marealle(1978) anafafanua kuwa mofu ni vipande vya neno ambavyo  husitiri mofimu. Kila mofu inamaana Fulani, Vipande hivyo vya maneno huwa na maana maalum katika kila neno hutegemeana na jinsi lilivyotumia.

N.B:  Kutokana na maana hizo tatu za mofu tunapata   mambo ya msingi kabisa ambayo hutumika kupambanua na dhana ya mofu. Pia kutokana na maana hizi tatu tunapata sifa za msingi zinazotumika kupambanua dhana ya mofu.

SIFA ZA MOFU

  1.       Mofu ni sehemu halisi ya neno

Mofu ni maumbo halisi ya maneno ambayo hutamkwa na watu wanapozungumza au kuandikwa, Kwa hiyo mofu ni  umbo halisi ambalo linaweza kusikika linapotamkwa na  linaweza kuonekana kwa macho ijapokua limeandikwa.

  1.       Mofu hudhihirika kifonolojia na kiathografia

Mofu ni umbo halisi la neno na kwa kuwani ni umbo halisi la neno basi mofu hudhihirika kifonolojia zinapotamkwa na kimaandishi zinapoandikwa.

  1.       Mofu huwakilisha maana

Kila mofu huwakilisha maana Fulani, Neno lolote lile katika lugha yoyote ile litakuwa na maana,

 Maana hiyo huwa imesitiriwa katika mofu zinazolijenga neno hilo.

 Hii ina maana kuwa kila neno lenye maana Fulani lazima maana hiyo itakuwa imewakilishwa na mofu Fulani. Pia hakuna neno lolote katika lugha yoyote ambalo litakauwa ni neno lenye maana bila kuwa na mofu angalau moja.

  1.       Mofu ni kipashio kidogo kabisa cha neno

Mofu ndiyo sehemu ndogo kabisa katika neno ambayo hubeba maana na sehemu hiyo haiwezi kugawanyika katika sehemu ndogo zaidi zilizo na maana. Mofu ni umbo ambalo ni kubwa kuliko fonimu lakini ni dogo katika neno.

N.B: Lakini katika lugha ya Kiswahili  wakati mwingine mofu hulingana  na neno. Mofu ni vile viambishi mbalimbali ambavyo huwa vinawekwa kwenye mzizi wa neno pamoja na mzizi wenyewe. Kila  kiambishi cha neno pamoja na mzizi wenyewe.Kila kiambishi cha neno ni mofu na mzizi wa neno pia ni mofu. Mfano:

Mofu huainishwa kwa kutumia vigezo vikuu viwili

  1.       Kigezo cha maana yaani maana zinazowakilishwa mofu
  2.       Kigezo cha mofolojia ya mofu

Kwa kutumia kigezo cha maana kuna aina tatu (3) za mofu

  1.       Mofu huru
  2.      Mofu funge
  3.     Mofu tata

Kwa kutumia kigezo cha mofolojia kuna aina kuu tatu (3)  za mofu

  1.       Mofu changamano
  2.      Mofu funge
  3.      Mofu tata

Kwa kutumia kigezo cha mofolojia kuna aina kuu tatu (3) za mofu

  1.      Mofu changamano
  2.     Mofu mzizi
  3.   Mofu kopa
  1.       MOFU HURU

Mofu huru ni mofu ambazo zinaweza kukaa zenyewe kama maneno yenye maana inayoeleweka bila kusaidiwa na mofu nyingine,

                       Mfano: Nomino (kaka) (paka) sungura)

Vivumishi (safi) (udhaifu)(hodari)  Imara) Zuri

Vielezi ((Haraka) (Juzi) Leo

Vitenzi (afiti) Samohe) Ariful)

Viunganishi (halafu) (pia) (ila)

  II. MOFU FUNGE

Hizi ni mofu ambazo haziwezi kutumika peke yake kama neno kamili  bali hutumika kama  kiambishi ambacho huambatana na mofu nyingine ili kukamilisha neno

Mofu funge inasifa mahususi

  1.       Haiwezi kusimama peke yake ikajitegemea kwa kawaida
  2.     Kwa kawaida mofu  funge ni  mofu   tegemezi hivyo  ni lazima iambatane  na angalau mofu nyingine moja  ili iweze kujitosheleza kimaana. Baadhi ya wanaisimu huiita mofu tegemezi
  3.       Maana ya mofu funge hutegemea muktadha wa mofu kimahusiano na mofu nyingine. Mofu tegemezi kazi zake huwa zimefungwa kwenye muktadha maalumu na zinapoondolewa kwenye muktadha huo hukosa maana na ni vigumu kujua bila kuweka katika muktadha wa neno.

Mfano; Kula – (ku) + (l) + (a)

             Kunjwa – (ku)  (nyw)  + (a)

            Mpe – (m) + (pe)

            Sikusoma – (si) + (ku) + (som) +(a)

Mofu  hizi ni  mofu tegemezi kwa sababu haziwi wazi kusimama zenyewe

III. MOFU TATA

 Hizi ni mofu ambazo huwa na maana zaidi ya moja na hivyo husababisha tungo kueleweka kwa namna zaidi ya moja

Mfano: Juma alimpiga John mpira

  1.       Juma alimpiga  mpira kwa kuelekezakwa John
  2.       Juma  alitumia mpira kama kifaa cha kumpigia Johari
  3.       Juma  alipiga mpira kwa niaba ya John
  4.       Juma alimpiga John kwa sababu  ya mpira

Maana hizi nne zimesababishwa na mofimu tata (-i-) Ambayo inajitokezakatika sentensi alimpigia

 

IV MOFU CHANGAMANO

 Hizi ni mofu ambazo huundwa angalau na mashina au mizizi miwili ya neno ambayo katika mazingira na kila mmoja hujitegemea,

Mfano: Kiona mbali Mofolojia ya neno hili ina uweo kutazamwa kwa namna kuu mbili

  1.       Namna ya kwanza: linaweza kutazamwa kama neno  lenye mofu tatu (3)

(ki-) + (on-) + (-a-) + (mbali)

  1.       Linaweza kutazamwa   kama neno  lenye mofu tatu (3)

(ki-) + (-on-) + (-mbali-)

(ki-) + (-onambali)

Katika neno kuona mbali kuna mizizi  miwili, linaweza kutazamwa kama neno moja lenye mzizi mmoja

(-onambali) hii ni mofu changamano kwa sababu huundwa na mizizi miwili ambayo katika  mazingira  mengine inaweza  kutenganishwa na kila mzizi kujitenga enyewe.

V. MOFU KAPA

Hizi ni mofu za  kipekee ambazo hazina umbo  hazitamkwi tunapozungumza wala haziandikiwi tunapoandika,  wala hazionekani kabisa  katika neno lakini athari za nafuu hizo  huwa  miongoni  mwa wazungumzaji.

NB:   Ingawa mofu kapa hazitamkwi wala kuandikwa, hazisikiki wala kuonekan kwa  macho lakini  maana  zake huwa zipo na tunazipata zinapotumika katika maneno ; kwa mfano tukichunguza maumbo ya  umoja  na wingi katika  majina  ya  Kiswahili, Majina hayo yanaweza  yakagawanywa  katika makundi mawili (2)

  1.        Ni  majina yenye maumbo dhahiri ya  umoja  na wingi

Mfano  m – pira      mi – pira

              m-ti            mi –ti

              ki – ti            vi – ti


ALOMOFU
.
Alomofu ni maumbo zaidi au maumbo tofauti ambayo huwakilisha mofimu moja kisarufi ambayo hufanya kazi moja kisarufi, alomofu hutokea mazingira maalum baadhi ya mazingira hutabirika mengine hayatabiriki kabisa. Alomofu kwa kawaida hubadili maana ya neno.

UTOKEAJI WA ALOMOFU
Mazingira ya kifonolojia (matamshi)

Mfano: Mtu anaposikia neno “funguo” anajua ni zaidi ya moja.

vi.   MOFU MZIZI

Mofu mzizi ni kiini cha neno.  Mofu mzizi ndio hubeba maana ya msingi katika neno. Mofu huwa haibadiliki neno linapoandikwa mofu nyingine

Mfano;(u) +(Funguo) na (wa) + (toto)

Funguo na toto ni mofu   mzizi

N:B Uainishaji wa aina hizo za  mofu huzingatia maana zinawakilishwa na mofu na kigezo kwa kigezo cha  kimofolojia.

TUNGO

Neno tungo hutokana  na kitenzi tunga,  Wanasema  hufasiri kuwa tungo ni matokeo ya kuweka  na kupanga  pamoja  vipashio vidogo ili kujenga vipashio vikubwa zaidi katika lugha. Katika sarufi tungo ndogo kuliko tungo nyingine  za neno ambalo huundwa kutokana na kuwekwa pamoja mofimu kuwa tungo kubwa kuliko nyingine zote ni tungo.

AINA ZA TUNGO

Katika  lugha ya Kiswahili kuna aina kuu  nne za tungo ambazo huainishaji  wake au mpangilio wake unazingatia  hali ya tungo. Tungo hizo hupangwa kuanzia tungo ndogo hadi kubwa zaidi,

1.      Tungo neno ambayo hujengwa na mofimu

2.      Tungo kirai ambayo hujengwa na maneno

3.      Tungo kishazi ambayo hujengwa na maneno au kirai

4.      Tungo sentensi ambayo hujengwa na tungo kirai au kishazi

1.      TUNGO NENO

Neno  ni mkusanyiko wa silabi , au  silabi  hutamkwa  au huandikiwa na kuleta maana

Mfano: Ng’ombe

             Tafiti

             Anatembea

             Taifa

N:B :   Neno hujengwa  na mofimu moja  au zaidi, Neno linalojengwa na mofimu  moja  huitwa neno sahili au huru na neno linalojengwa na mofimi zaidi ya moja huitwa  neno changamoto. Maneno mengi katika  lugha ya Kiswahili ni changamana,

AINA ZA MANENO

Wataalamu wa lugha ya Kiswahili wanatofautiana katika uainishaji wa aina za maneno. Wapo ambao wanaainisha aina saba (7) tu za maneno katika lugha ya  Kiswahili na wengine  huainisha aina nane (8) za aina za maneno. Wataalamu wanoainisha aina saba za maneno F. Mkwera (1978), Kapinga (1983) TUMI (1988) Mohamed (1986), Msamba na wanzake (1999) Kihore na wenzake (2001) wataalamu wengine wameainisha aina nane za maneno. MbundaMsokile (1992), J.S Mdee (1988), Ngullu R. (1999), Y. Rubanza (2003), MBadu (2000)

Wataalamu wanaoainisha aina nane za maneno hutofautisha dhana ya kiunganishi  na  kihisishi lakini wale wanaoainisha aina saba za maneno huona kuwa dhana hizo ni dhana mbili zinazofanana.

1.      NOMINO /MAJINA (N)

Majina ni aina ya  maneno ambayo hutaja vitu, viumbe, hali au matendo ili kuviainisha  na kuvitofautisha  na vitu vingine.

Mfano: Winnie, Werevu, Wema, Lulu, Mtu, Ubungo, Mungu na n.k

AINA ZA MAJINA

a.Majina ya kawaida

Majina haya yanataja viumbe kama vile wanyama, miti, watu, ndege, wadudu.

 Majina  yote  hayo  yanapoandikwa  huanza  kwa herufi ndogo kama yanatokea  katikati ya sentensi au tungo.

N:B  Majina  hayo  sio maalumu kwa  vitu  Fulani tu bali kwa vitu mbalimbali.

b. Majina ya  Pekee.

 Haya ni majina maalumu  kwa watu au mahali ambaye huonesha upekee kwa watu,mahali au vitu, Majina haya hujumuisha majina binafsi ya watu na majina ya mahali.

Mfano: Marcus, Halima, James, Abel, Fredy, Anna Ubungo, Manzese, Tanzania, Uingereza, Africa

N: B Majina hayo yanapoandikwa huanza kwa herufi kubwa

C. Majina ya jamii.

Haya ni majina ambayo yanataja vitu au watu wakiwa katika makundi au mafungu japo huwa majina hayo yapo katika hali ya umoja. Mfano, Chama , kamati, kadamnasi, timu

d. Majina dhahania

Haya ni majina yanayotaja dhana zinazofikirika zisizonekana kwa macho wala kushika

Mfano:Afya, utajiri, upole ukatili, Mungu, shetani, malaika, Majina yote hao yanapandikwa yapo ambayo huanzia herufi kubwa hata kama huandikwa katikati ya sentensi

e. Majina ya wingi

Haya ni majina ambayo yanadokeza dhana ya  wingi japokuwa majina haya hayana umoja  wala umbo la majina haya hufanana na majina  yaliyopo kwa wingi ingawa mfanano  huo hauwiani moja kwa moja na majina ya wingi, Majina hayo  umoja na wingi wake  hudhihirika kutokana na  upatanishi kisarufi uliopo baina ya majina  hayo na vitendo

Mfano: wa majina hayo ni kama vile maziwa,mazungumzo, marashi, maji, mafuta manukato, madhehebu.

N:B Majina haya huwa hayana umoja wala wingi japokuwa baadhi ya wazungumzaji huwa wanalazimisha. Dhana ya wingi huwa inadhihirishwa na upatanishi wa kisarufi

Mfano: Maziwa yameharibika

             Maziwa mengi yameharibika

             Mafuta yamemwagika

             Mafuta mengi yamemwagika

II. KIWAKILISHI (W) Kibadala /vijina)

Huwa ni maneno ambayo hutumika badala ya jina au ni maneno ambayo huwakilisha jina. Aina hii ya maneno huwa haitokei kama majina yametumika bali hutokea endapo tu majina hayapo.

N:B  Viwakilishi haviwezi kutokea pamoja na majina katika sentensi

        Mfano:   wewe ni mzuri

                                          W

        Wao wanaogopa matokeo

  W

        Wangapi  watafaulu mtihani

   W

        Huyu aliyekuja amefaulu mtihani

    W

AINA ZA VIWAKILISHI

Kuna aina kuu tano za viwakilishi katika lugha ya Kiswahili, ingawa baadhi ya wanasarufi huainisha viwakilishi zaidi ya hivyo,

a.      Viwakilishi vya nafsi

Hivi ni viwakilishi ambavyo hutaja nafsi au huwa kilisha nafsi mbalimbali.

        Mfano;

        Mimi ninasoma (nafsi ya kwanza umoja)

                       W

        Sisi tunasoma (nafsi ya I wingi)

                       W

        Wewe  unasoma  (nafsi ya II umoja)

                        W

        Yeye anasoma (nafsi ya  III umoja)

                         W

        Wao wanasoma (nafsi ya III wingi)

                       W

b.      Viwakilishi vya Mahala/ vioneshi

Hivi ni viwakilishi ambavyo huonyesha kitu kilipo

           Mfano: Hawa ni wafanyakazi wa St. Mery Goreti

                          W

            Huyu ni mlevi sana

             W

             Yule ni mtoto

             W

C. Viwakilishi viulizi

Hivi ni viwakilishi ambavyo hutumika kuuliza swali ambalo hurejelea  kwenye nomino husika

        Mfano:    Lipi linakuchanganya

                                       W

                       Wangapi wamefaulu?

                            W

d.Viwakilishi vimilikishi

  Hivi ni viwakilishi ambavyo huonesha umiliki ambao huvumishwa moja kwa moja na nomino inayohusika

                         Mfano: Kwetu pazuri

                                         W

 Wangu ninampenda

                                       W

Kwenu ni pazuri

                                       W

e. Viwakilishi vya  kurejesha

Hivi ni viwakilishi ambavyo hurejesha tendo kwa mtenda au mtendwa na mara nyingi huundwa na mzizi wa amba – pamoja na viambishi vya urejeshi

    Mfano:    Ambao wamechelewa wameadhibiwa

                                       W

                                     Ambazo zimejengwa barabarani zibomolewe

                                        W

                                    Ambavyo vimeharibika vitupwe

                                       W

                                   Aliyepotea amepatikana

                                       W

III  VIVUMISHI (V)

Vivumishi ni maneno au kikundi cha maneno ambacho hutoa maelezo zaidi kuhusu nomino au kiwakilishi. Vivumishi ni maneno yanayovumisha majina au viwakilishi vilivyomo katika tungo. Maelezo hayo ambayo huumbwa na majina  yanaweza kuwa na tabia ya jina au idadi ya jina n.k

AINA ZA VIVUMISHI

 Wataalamu  wa sarufi ya  Kiswahili wanatofautiana  na katika uainishaji wa aina  za vivumishi lakini  pamoja na kutofautiana huko wanaonekana kukubaliana  katika aina  kuu nane (8) za vivumishi

a.      Vivumishi vya idadi

Hivi ni vivumishi ambavyo huonesha idadi ya vitu watu au majina mengine yaliyotajwa.  Vivumishi hivi huweza kutaja idadi ya vitu waziwazi lakini wakati mwingine hutaja idadi ya  vitu katika orodha,

Mfano: Mikate mitano

                           V

            Watu wengi

                          V

          Ghorofa ya kumi

                          V

          Chai kidogo

                          V

          Maji mengi

                       V

b.      Vivumishi vya sifa

Hivi ni vivumishi vinayosifia majina wakilishi vilivyopo katika tungo

Mfano:  Mkulima hodari

                                 V

              Msichana mrembo

                                   V

              Nchi masikini

                                V

              Uchumi dhaifu

                                 V

c.      Vivumishi vya kumiliki

Hivi ni vivumishi ambavyo   huonesha umiliki wa kitu watu au wanyama

Mfano:  Kitabu changu

                              V

              Shule yake

                          V

Vivumishi vioneshi
Hivi ni vivumishi vinavyoonesha mahali kitu kilipo au mtu alipo huitwa vivumishi vya mahali kwa sababu vinaonesha mahali.
Mfano: Mtoto huyo.

              V

Mtoto huyo
V
Mtoto yule
V

Vivumishi viulizi
Hivi ni vivumishi amabavyo huuliza ili kupata idadi ya watu au vitu.
Mfano: Vitabu vingapi vimenunuliwa?

                             V

Kiongozi gani amekuja?
V

Vivumishi vya jina kwa jina
Hivi ni vivumishi amabavyo huwa ni majina yanayovumisha au kutoa maelezo zaidi kuhusu majina mengine.
Mfano: Mtoto kiziwi
V

Mpenzi jini
V

Mpenzi bubu
V

Mzee bubu
V
Vivumishi vya a-unganifu.
Hivi ni vivumishi ambavyo huwa na jina lenye-a-ya uunganifu.
Mfano: Mambo ya kihuni
V

Chakula cha watoto.
V

Nguo za kichina
V

Vivumishi vya pekee.
Hivi ni vivumishi ambavyo huonesha ziada ya kitu, mtu au jina lolote lililotajwa.
Mfano: Mtu mwenyewe haeleweki
V
Sisi sote ni ndugu
V
Ninyi nyote ni wanafunzi
V

VITENZI
Kitenzi ni neno ambalo hutaja jambo lilitendwa, linalotendwa au litakalotendwa na kitu, mtu au kiumbe chochote kile chenye uwezo wa kutenda tendo husika. Aidha kitenzi huonesha tabia au hali inayoweza kuwepo au kutokuwepo kwa mtu, kitu au kiumbe kingine chochote kile.

NB; Katika lugha ya kiswahili vitenzi huwa havitumiki pekeake bali huambatana na viambishi ambavyo hudokeza nafsi ya mtendwa au mtenda, wakati tendo lilipofanyika pamoja na kauli ya tendo.
mfano:
Kula – Anakula

Vivumishi vioneshi

c.       Hivi  ni vivumishi vinavyoonesha  mahali, kitu kilipo au mtu alipo huitwa vivumishi vya mahali kwa sababu vinaonesha mahali.

        Mfano: Mtoto huyo

                V

        Mtoto huyo

             V

        Mtoto Yule

              V

        Yule  mtoto amepotea

   V

e. Vivumishi viulizi

Hivi ni vivumish ambavyo huuliza  ili kupata idadi ya watu au vitu

Mfano: Vitabu  vingapi vimenununuliwa?

                              V

              Kiongozi gani amekuja?

                                V

f. Vivumishi vya jina kwa jina

Hivi ni vivumishi ambavyo huwa ni majina  yanayovumisha   au  kutoa  maelezo zaidi kubuni  majina mengine

Mfano: Mtoto  kiziwi

                            V

            Mpenzi jini

                           V

            Mpenzi Bubu

                          V

            Mzee bubu

                       V

g.    Vivumishi vya  a- Unganifu

Hivi ni vivumishi ambavyo huwa na  jina lenye- a – ya uunganifu

Mfano: Mambo ya kihuni

                                 V

             Chakula cha watoto

                             V

            Nguzo za kichina

h.    Vivumishi vya pekee

Hivi ni vivumishi ambavyo huonesha ziada ya kitu, mtu au jina lolote lililotajwa

Mfano: Mtu mwenyewe haeleweki

                         V

             Sisi sote ni ndugu

                       V

            Ninyi nyote ni wanafunzi

                         V

IV. VITENZI

 Kitenzi ni neno ambalo hutaja jambo lililotendwa, linalotendewa, au litakalotendwa na kitu, mtu au kiumbe chochote kile chenye uwezo wa kutenda tendo husika. Aidha kitenzi huonyesha tabia au hali inayoweza kuwepo au kutokuwepo kwa mtu, kitu au kiumbe kingine chochote kile.

N.B: Katika lugha ya Kiswahili vitenzi huwa havitumiki peke   yake bali huambatana na viambishi ambavyo hudokeza nafsi ya mtendwa au mtenda, wakati tendo lilipofanyika pamoja na kauli ya tendo.

Mfano:

             Lala – Anaimba

             Kula – Anakula

AINA ZA VITENZI

Wataalamu wa lugha ya Kiswahili wanatofautiana katika uanishaji wa aina za vitenzi, wapo wanaoainisha aina kuu tatu (3) yaani kitenzi kikuu (T) kitenzi kisaidizi (Ts) na kitenzi kishirikishi (t). na wapo wanaoainisha aina  kuu (2) yaani kitenzi halisi na kitenzi kishirikishi

N.B Katika uainishaji wa vitenzi, tutashughulikia uainishaji wa aina kuu mbili (2) za vitenzi yaani vitenzi halisi na vitenzi vishirikishi.

a.      Kitenzi halisi

Hivi ni vitenzi ambavyo hueleza matendo. Katika lugha ya Kiswahili kitenzi  halisi kinaweza kutumika  kimoja au zaidi ya kimoja katika sentensi. Vitenzi vinapotumika humbatana na viambishi ambavyo hudokeza nafsi  wakati halisi au kauli ya tendo na  hivyo kwa pamoja  hufanya kifungu tenzi halisi.

Aina za   vitenzi halisi

Kuna  aina kuu mbili (2) za  vifungu tenzi halisi

–         Kifungu tenzi halisi kikuu (T)

–         Kifungu tenzi halisi kisaidizi (TS)

1. kifungu tenzi  halisi kikuu (T)

  Hiki ni kifungu tenzi ambacho hueleza tendo lililofanywa, litakalofanywa  au linalofanywa na mtendo au tendo alilofanyiwa, analofanyiwa au atakalofanyiwa mtendwa kutokana na sifa  hii vitenzi hubeba nafsi ya mtenda,  mtendwa wakati tendo lilipofanya pamoja. hali  kauli ya tendo sifa hizi huzifanya kitenzi kuwa aina ya neno inayobebeshwa mzigo mkubwa katika lugha ya Kiswahili.

        Mfano: Juma alikula chakula

                         T

        Juma  anakula chakula

               T

        Juma atakula chakula

               T

II. KIFUNGU TENZI HALISI KISAIDIZI  (TS)

Hiki ni kitenzi ambacho huambatana na kitenzi halisi kikuu na aghalabu huoneshwa wakati tendo lilipofanyika na pia hudokeza uyakinishi au ukanushi wa tendo.  Kifungu tenzi halisi kisaidizi hutumika sambamba na kifungu tenzi halisi kikuu.

 Kikitumika peke yake bila kuambatana na kitenzi kikuu basi dhima yake hubadilika na kuwa kitenzi kikuu kikiondolewa katika tungo, Kitenzi kisaidizi huchukua dhima ya kitenzi kikuu.

Mfano:  Juma anataka   kula chakula

                           Ts          T

               Juma anataka chakula

                            T

 

N.B:    Katika sentensi ya pili kitenzi  anataka kimechukua dhima ya kitenzi kikuu baada ya kuondoa  kitenzi  kile ambacho kilikuwa kitenzi kikuu katika sentensi ya kwanza. Pia vitenzi visaidizi vinaweza kutumika zaidi  ya kimoja  katika  sentensi  visaidizi vinaweza kutumika zaidi ya kimoja katika  sentensi.

        Mfano: Juma alikuwaanataka kwenda kusoma

                             TS       TS           T

b.      Kitenzi kishirikishi (t)

Haya ni maneno yanayoonyesha tabia au hali Fulani iliyopo kwa mtu au kitu Fulani vitenzi vishirikishi ambavyo huonesha tabia au hali Fulani iliyopo kwa mtu au kitu huitwa vitenzi vishirikishi yakinishi. Na vitenzi vishirikishi ambavyo huonesha kutokuwepo kwa hali au tabia kwa mtu au kitu huitwa vitenzi vishirikishi vikanushi.

N:B Mara nyingi katika lugha ya Kiswahili kitenzi kishirikishi yakinishi ni “ni” na kitenzi  kishirikishi ni   na kitenzi kishirikishi kanushi “si” Lakini kuna vitenzi vingine  vishirikishi zaidi  ya hivyo katika lugha ya Kiswahili

Mfano

        Juma  ni   mtoto
t

        Juma   si    mtoto
t

        Juma siyo mwizi
t

        Udongo  u  mkavu
t

        Babu   yu  mkali
t

        Kitabu   ki   kidogo
t

        Mchungwa   u   mkubwa
t

        Midomo i minene
t

        Ubao   u  mpana
t

        Mbao zi pana
t

         Hapa pa pachafu
t

        Huku  ku  kuzuri
t

        Humu  mu  mweusi
t

        Chakula   ndicho  kitamu
t

        Anna   ndiye  mgonjwa
t

        Juma  angali mtoto
t

        Wanafunzi hawa wangapi wadogo
t

Maneno yote yaliyopigiwa mstari ni vitenzi vishirikishi

KAULI  ZA VITENZI

Vitenzi vya lugha  ya Kiswahili vinatabia ya kunyumbuka  na hivyo kuzalisha kauli mbalimbali za vitenzi. Kauli hizo ni kama zifuatazo

Mfano:

ii.     Kauli ya kutendwa

Mfano:    Pigwa

                 Somwa

                 Limwa

                 Chezwa

iii.     Kauli ya kutendeka

Mfano:     Pigika

                 Valika

                  Someka

                  Limika

iv.   Kauli ya  kutendana

Mfano:     Pigana

                  Vaana

                  Toana

                  Somana

v.      Kauli ya kutendana

Mfano:    Iimiana

                 Someana

                 Valiana

                 Toleana

vi.   Kauli ya kutendechwa

Mfano:   Shoneshwa

                 Someshwa

                 Limishwa

                 Valishwa

vii.             Kauli ya kutendea

Mfano:      Pigia

                  Somea

                 Limia

                 Zalia

viii.          Kauli ya kutendwa

Mfano:    Pigiwa

                 Somewa

                 Shonewa

                 Chezewe

HALI ZA TENDO

Vitenzi vya lugha ya Kiswahili vinavyotumika huweza   kuonesha hali tofauti kutokana na kuambishwa viambishi tofauti. Baadhi ya hali katika vitenda hujitokeza zaidi katika mazungumzo na nyingine mara chache

      i.  Hali ya masharti

Hali hii huonesha kuwa kufanyika kwa tendo Fulani sharti kutanguliwe na tendo lingine. Lazima kuwa na matendo mawili yaliyofuatana.

Mfano: Wangecheza kwa umakini wangepata ushindi

             Akija nitamwambia

ii.     Hali ya kuendelea kwa tendo

Hali hii huonekana katika tendo ambalo linaendelea kufanyika hili huziirishwa na mofu ya wakati “na” ambayo hupachikwa katika vitenzi.

Mfano: Anasoma

              Anakula

N: B    Pia hali ya kuendelea kwa tendo inaweza ikadokezwa na kiambishi “ki” ambacho aghalabu hutokea katika kitenzi cha pili katika sentensi yenye vitenzi sambamba.

Mfano: Aliniona nikisoma

N.B: Pia hali ya kuendelea kwa tena hudokezwa na kiambishi “Ka” katika masimilizi ya matendo yoliyofululizana katika masimulizi ya matukio mbali mbali, yaliyofanyika   moja baada ya jingine kimsingi yalipaswa kutumia kiambishi “li”ambacho hudokeza wakati uliopita lakini matumizi yake humchosha msemaji na msikilizaji lakini pia ni kwa kurudia rudia na kurejesha sentensi bila sababu hivyo kiambishi “ka” hutumika badala ya “li”

 

Mfano: Tulifika chuoni tukapokelewa na mkuu wa chuo, akatupa funguo za bweni akatuonesha pakulala na katupa magodoro na mablanketi akatupeleka kafteria.  Akatugawia sahani vijiko na visu akaagiza tugewe chakula kisha tukaenda kulala

iii.   Hali ya mazoea

Hii ni hali inayoonesha kujirudia rudia kwa tendo au mazoea ya kufanya tendo Fulani

Mfano: Baba huamka asubuhi na mapema

             Juma hucheza mpira wa miguu

N.B:  Hali ya mazoea hudokezwa na kiambishi “hu”

iv.   Hali timilifu

Hali timilifu katika vitenzi huonyesha kukamilika kwa tendo yaani tendo limekwisha kufanyika lakini athari za tendo hilo bado zinaonekana, kiambishi kinachotakiwa cha hali timilifu ni “me” katika hali ya uyakinishi katika hali ya ukanushi ni “ja”

Mfano:

        Juma amekimbia

        Juma hajakimbia

        Wazazi wake wamehama Tanga

        Mama hajapika chakula

 

v.                  Hali ya kuamuru (amri)

Hii ni hali ambayo hujitokeza katika kifungu tenzi na kawaida hudokezwa katika vitenzi na kiambish tamati “a” katika umoja nakiambashi tamati “eni” katika wingi paispo kumbatana na viambishi vya wakati.

Mfano:    Umoja              Wingi

                 Soma                 Som – oni

                 Tokea               Tok – eni

vi.               Hali ya kuhimiza

Hii ni hali ambayo hujitokeza kwenye vifungu tenzi kwa lengo la kusihi, au kumuomba mtu afanye jambo Fulani au asifanye jambo Fulani. Hali ya kutimiza hudokezwa na kiambishi “e” ambacho huwekwa mwishoni mwa kitenzi kwenye vitenzi vinayohusu nafsi ya kwanza umoja kwa vitenzi vinayohusu nafsi ya kwanza wingi hali ya kuhimiza huoneshwa na kiambish tamati “eni” ambacho huwekwa mwanzoni mwa kitenzi.

Mfano

Nilal-e

Niend –e

Tuend-eni

 

vii.             Hali ya kutarajia

Hali huonesha matarajio ya kutendeka kwa jambo pasipo kuwa na uhakika wa kutimia kwa nia hiyo

Mfano:

Nipende

Tupendane

N.B: Hali ya kutarajia pia hudokezwa na kiambishi tamati “e”

ALAMA ZA WAKATI KATIKA  KITENZI

Maranyingi vitenzi katika lugha ya Kiswahili huambatana na viambishi mbalimbali ambavyo hudokeza dhana mbalimbali na hivyo kufanya kazi kama kifungu tenzi. Kwa ujumla lugha ya Kiswahili ina nyakati kuu tatu zinazotumika zaidi yaani wakati uliopita wakati uliopo na wakati ujao. Nyakati hizi hudokezwa na viambishi mahususi vya   matendo yanapokuwa katika yakinifu na yanapo kanushwa.

        WAKATI  ULIOPITA

Wakati uliopita katika lugha ya Kiswahili hudokezwa na viambishi “–li” vitenzi vinapokuwa katika uyakinishi na kiambishi –ku- vitenzi hukanusha. Viambishi hivyo hutanguliwa na viambishi vingine kama vile viambishi vya nafsi na vya ukanushi.

Mfano:

Ni-li-kula                             si-ku-la

Tu-li-kula                             ha- tu- kula

U-li-kula                               hu-kula

M-li-kula                              ha-m-kula

A-li-kula                              ha-kula

Wa-li-kula                            ha-wa-kula

Ni-li-soma                            si-ku-soma

Tu-li-soma                            ha-tu-ku-soma

U-li-soma                             hu-ku-soma

M-li-soma                             ha-m-ku-soma

A-li-soma                             ha-ku-soma

Walisoma                             ha-wa-ku-soma

N:B  Hata hivyo vitenzi vya mzizi wa silabi moja huwa  wakati uliopita vitenzi hivyo vinakuwa  katika ukanushi kwa sababu ya athari za  kimatamshi

        WAKATI   ULIOPO

Wakati uliopita huonesha tendo linaloendelea kufanyika na kiambishi kinachodokeza wakati uliopo ni –na-“vitenzi vinapokuwa katika ukanushi  kiambishi –i- hupachikwa mwishoni mwa vitenzi.

Mfano:

Ni-na-kula                             si-l-i

Tu-na-kula                           ha-tu-l-i

U-na-kula                             hu-l-i

M-na-kula                            ha-m-l-i

A-na-kula                           ha-l-i

Wa-na-kula                          ha-wa-l-i

        WAKATI ULIOPO TIMILIFU

Wakati timilifu katika lugha ya Kiswahili hudokezwa na mofimu –me- vitenzi vinapokuwa ktika uyakinishi na mofimu –ja- vitenzi vinapokuwa katika ukanushi

Mfano:                      ni-me-soma           si-ja-soma

Tu-me-soma         hu-tu-ja-soma

U-me-soma           hu-ja-soma

A-me-soma            ha-ja-soma

Wa-me-soma         ha-wa-ja-soma

V. VIELEZI (E)

Vielezi  ni aina ya maneno ambavyo hutoa maelezo  zaidi  kuhusu kitenzi, kielezi mara nyingi hujibu  maswali kama tendo limefanywa  mara ngapi ? tendo limefanywa namna gani ?  tendo limefanywa lini ? na wapi ?

AINA YA VIELEZI

Vielezo vipo vya  aina kuu tano

a.      Vielezi vya namna /jinsi

Hivi ni vielezi ambavyo huonesha namna ambavyo tendo lililofanywa, linavyofanywa  au  litakavyofanywa

Mfano;    Wanafunzi wanasoma kwa bidii

                  Mwizi alipigwa sana

                  Nilimuona kwa macho yangu

b.      Vielezi vya idadi/kiasi

Hivi ni vielezi ambavyo hueleza kiasi ambacho tendo limefanyika, mfano tendo limefanyika mara nyingi au mara chache

                             Mfano: Debe limejaa pomoni

                                                                        E

Alianguka chini mara tatu

                                   E

Anaenda shuleni mara chache sana

                                      E

c.      Vielezi vya mahali/vioneshi

Hivi ni vielezi ambayo hueleza mahali ambapo tendo limefanyika

Mfano: Tuliambiwa twende darasani

                                                    E

                        Juma anaishi Arusha

                                                   F

                      Mwalimu amekwenda nyumbani

                                                           E

d.      Vielezi vya wakati

Hivi vielezi ambavyo hudokeza muda au wakati tendo lilipofanyika

Mfano: Mvua imenyesha usiku kucha

                                                      E

Njoo kesho asubuhi

            E

Tutafanya mtihani Alhamisi

                                    E

e.      Vielezi viingizi

Hivi ni vielezi ambavyo hueleza tendo lilivyofanyika kwa kuigiza au kufuatisha mlio wa sauti unaajitokeza wakati tendo husika inapotendeka

Mfano:      Mbwa alilia bwe

                                         E

                  Alidondoka chini puu

                                                 E

N: B    Jambo la msingi la kuzingatia katika vielezi ni kwamba kielezi uhusiana na kitenzi, kielezi hutokea baada ya kitenzi au baada ya shamirisho na wakati mwingine kielezi kinaweza kutanguliwa kabla ya kitenzi.

Mfano: Juma anacheza mpirauwanjani

                                          Sh         E

            Juma anacheza uwanjani

                                           E

            Aliponiona alikimbia

                     E

VI. VIIGIZI/VIINGIZI/VIHISISHI (J)

Haya ni maneno yanayodokeza vionjo au miguso ya moyoni au akilini aliyokuwa nayo mzungumzaji. Viingizi hudokeza hisia kama vile za furaha,   huzuni, uchungu, kushangaa, kushtuka, laana, matumaini au kukata tamaaa, huruma na n.k

Mfano:          Ebo! unaumwa nini?

                           I

Yanga zii!

             I

Lah!  Naipenda kweli

    I

Mmh!  We hujui tu

   I

N.B:    vihisishi mara nyingi vinapotumika katika maandishi huambatana na alama ya mshangao

VII. VIUNGANISHI (U)

 Ni maneno au kikundi cha maneno, chenye kuunganisha kirai, kishazi au sentensi.

Dhima kubwa ya viunganishi ni kuunganisha vipashio viwili au zaidi vyenye hadhi sawa kisarufi. Mfano: Jina na jina kishazi na kishazi, kitenzi na kitenzi, sentensi na sentesi

Mfano;          Shangazi na mjomba wanapendana sana

                                       U

Aje  Juma au Hamisi

n                  U

Vitabu vyote  vya  mama  yangu

                                                 U

 

AINA ZA VIUNGANISHI

Viunganishi vinaweza vikagawanywa katika makundi makuu mawili

a.      Viunganishi huru

Hivi ni viunganishi ambavyo husimama peke yake katika tungo au vipashio vinavyounganishwa.

Kiungo huru kinaweza kutoka katikati ya tungo mbili zinazoziunganisha au mwishoni mwa tungo mbli zinazoziunganishwa

Mfano:   Nitukane tu lakini nakupenda

                                        U
                  Hata ukinitukana nakupenda

                      U

AINA ZA VIUNGAISHI HURU

Viunganishi huru vinaweza  vikagawanywa katika makundi madogo madogo.

a.      Viunganishi huru nyongeza

Hivi ni viunganishi ambavyo huelekeza dhana ya kuongezwa idadi ya vitajwa au matendo yanayosimuliwa

Mfano:    Juma na zaina wanaondoka   kesho

                            U

Aliiba chakula kisha akaiba na sahani

                                            U

b.      Viunganishi huru chague

 

Hivi ni viunganishi huru ambavyo hudokezwa maana ya uchambuzi wa vitajwa au matendo

Mfano:    Sinywi pombe wala kuvuta sigara

                                              U

Utaondoka leo ama kesho

                          U

c.      Viunganishi huru linganishi

Hivi ni viunganishi ambavyo hudokeza hali ya kulinganisha iliyopo katika tungo mbili au zaidi

Mfano:    Nakupenda ingawa hunitaki

                                          U

Juma hakufaulu sembuse  Ali afaulu

                               U

Aliondoka mapema lakini alichelewa kufika

                                  U

d.      Viunganishi huru sababu

Hivi ni viunganishi ambavyo hudokeza sababu au matokeo ya matendo yaliyofanyika

Mfano: Alifeli mtihani kwa sababu hakusoma

Ijapokuwa nakupenda usininyanyase

Unaongea kama hutaki

-Iliopigiwa mstari ni viunganishi.

AINA ZA VIUNGANISHI TEGEMEZI

Hivi ni viunganishi ambavyo huwa na kiambishi cha O – ya urejeshi ambayo huwekwa katika kitenzi cha kishazi tegemezi ili kukiunganisha na kitenzi kikuu cha kishazi huru ambavyo kwa pamoja huunda sentensi changamano.

N.B Viambishi tegemezi huwa ni viambishi, lakini wakati mwingine pia huweza kuwa ni maneno maalumu. Pia viunganishi tegemezi vinawezakutokea mwanzoni mwa tungo mbili zinazounganishwa

Mfano:          Aliponiona alikimbia

                              U

Chakula kilichobaki kimechacha

                                   U

Katika sentensi hizo viunganishi tegemezi ni –po- na – cho-, ambapo kiunganishi –po- kinaunganisha chakula kilibaki na chakula kimechacha.

Wakati mwingine pia viunganishi tegemezi huweza kujitokeza kama maneno

Mfano:           Ijapokuwa nilimkataza alimpiga

                               U

Ingawa hakusoma alifaulu

     U

VIII VIHUSISHI (H)

Haya ni maneno yanayoonesha uhusiano baina   ya tungo mbili zenye maadhi tofauti kisanii

Mfano:          Uhusiano kati ya kitenzi na jina

Anatembea kwa miguu

                     H

Anakula kwa kijiko

                H

Simama mbele ya nyumba

                 H

Huyu ni mtu mwenye maneno  mengi

                       H

N:B:   Baadhi  ya wanasarufi huchanganya dhana ya viunganishi na vihusishi  lakini ukweli ni kwamba dhana ya viunganishi na vihusishi hutofautiana. Tofauti hii hutokana na dhima ya dhana hizo katika  tungo. Kwamba dhima ya viunganishi ni kuunganisha tungo zenye hadhi sawa kisarufi wakati dhima  ya vihusishi ni kuonesha uhusiano uliopo baina ya  tungo mbili zenye hadhi tofauti kisarufi.

AINA ZA VIHUSISHI

a.      Vihusishi vya Mahala

Ni vile ambavyo huonesha uhusiano wa Mahala baina ya tungo mbili

                 Mfano    Aliweka katika sanduku

                                                    H

Alikaa mbele ya mlango

    H

b.      Vihusishi vya wakati

Hivi huonesha uhusiano wa wakati baina ya tungo mbili

         Mfano:  Alifika baada ya masaa  machache

                                       H

c.      Vihusishi vya sababu

Hivi huonesha sababu au uhusiano uliopo kwa kutokea kwa jambo Fulani baina ya tungo mbili

Mfano: Alipigwa kwa ajili ya makosa yake

                                     H

d.      Vihusishi vya ulinganishi

Hivi huonesha uhusiano wa kimlinganisho baina ya tungo mbili

Mfano: Ng’ombe ni  mmoja kuliko mbuzi

                                                  H

e.      Vihusishi vya namna au jinsi

Hivi vinaonesha uhusiano wa kinamna baina ya tungo mbili

Mfano: nataka maji ya moto

                                         H

f.       Vihusishi vimilikishi

Hivi honesha uhusiano wa kumiliki baina ya tungo mbili

Mfano: Aliiba fedha za kanisa
H

g.      Vihusishi vya ala (chombo kilichohusika)

Hivi huonesha uhusiano uliopo baina ya tendo na kitukilichotumika katika tendo hilo

Mfano: Alipigwa kwa fimbo
H

Maswali

1.      Nini tofauti kati ya viwakilisi na majina?

2.     Kuna uhusiano gani kati  ya nomino na vivumishi  au viwakilishi na vivumishi

3.     Vitenzi  vishirikishi katika lugha ya Kiswahili si vingi lakini ni muhimu jadili

4.      Si kila kiambishi huambatana na mzizi kwa  namna ile ile   jadili kwa mifano

5.       Kuna tofauti gani kati ya  tungo na sentensi?

6.       Kirai ndiyo msingi wa  muundo wa tungo nyingine Thibitisha kwa mifano

7.       Vivumishi katika lugha ya kiswahihi havina uhai nje ya umbo la kirai nomino thibitisha kwa mifano.

2.      KIRAI/KIKUNDI

Kirai ni kipashio au tungo yenye neno moja au zaidi lakini isiyokuwa na muundo wa kiima na kiarifu. Muundo wa kiima  na kiarifu ni muundo uoneshe  mtenda na jambo linalotendwa au mtendwa  wa jambo na jambo analotendwa.  Kuna miundo mbalimbali ya kirai ambayo uhusisha neno moja au zaidi ambayo huwekwa kwa pamoja kwa kuzingatia mpango maalumu ambao huzingatia uhusiano baina ya neno kuu na maneno mengine ambayo huambatana na neno kuu.

Mfano: Kirai nomino

Katika kirai nomino neno kuu ni nomino hivyo muundo wake umekitwa kwenye nomino na neno au fungu la maneno.
Mfano: Mtoto yule mwembamba
KN
Miti ile mitatu mirefu
KN

SIFA ZA KIRAI

Kirai kina sifa mbalimbali ambazo hukifanya kirai kiweze kutambulika kiurahisi

i.    Kirai hakina kiima na kiarifu muundo ambao huonesha mtenda na jambo analolitenda, tungo nyingine ni neno, kishazi na sentensi

ii   Kirai hujengwa na neno moja  moja au zaidi ya moja kwa kuzingatia  uhusiano uliopo baina ya neno  kwa  maneno mengine

iii  Hutegemea uhusiano maalumu baina ya neno,  na maneno mengine yanyohusiana na neno kuu (uainishaji wa virai)

Mfano: Katika kirai nomino neno kuu ni nomino katika kirai kiunganishi neno kuu ni kiunganishi.

iV.   Kirai huweza kutokea upande wa kiima au kiarifu katika sentensi

V.     Kirai ni tungo kubwa kuliko neno,  lakini ndogo kuliko kishazi

AINA ZA VIRAI

Kuna aina kuu tano za virai. Ambazo ni

1.      Kirai nomino (KN)

2.      Krai kivumishi (KV)

3.      Kirai kitenzi (KE)

4.      Kirai kielezi (KE)

5.      Kirai kiunganishi (KU)

1. KIRAI NOMINO

ni kirai ambacho muundo wake umekitwa kwenye mahusiano ya nomino na maneno mengine na nomino na maneno mengi ambayo yanamahusiano na  nomino. Neno kuu katika kirai nomino ni nomino ambayo ndiyo msingi mkuu wa mahusiano na maneno mangine.

MIUNDO YA KIRAI NOMINO

Kirai nomino kina miundo mbalimbali

      I.Muundo wa nomino peke yake

Mfano: Cbaki)

             Baba

             Mama

             Winnie

b.      II.Nomino  mbili  au zaidi  zilizounganishwa

Mfano:    Baba na mama

                 Baba na bibi

                 Babu na bibi

                 Mwalimu na wanafunzi

                 Mjomba na shangazi

       III.Muundo wa nomino na kivumishi kimoja au zaidi

Mfano: Mtoto Mweusi

             Watoto wanene wazuri

             Watoto na shangazi

IV. Muundo wa nomino na kivumishi kimoja au zaidi

    Mfano:  Yule mtoto

                   Watoto wake watatu wanene wazuri

d.    V. Muundo wa  kivumishi na jina

Mfano:  Yule mtoto

              Kile kitabu
VI.  Nomino na kishazi tegemeza kivumishi

Mfano: Mbwa aliyepata kichaa

f.    VII.   Nomino ,  kivumishi  na kishazi tegemezi kivumishi

Mfano: Msichana Yule mrembo uliyeniona naye jana

g.      VIII.Nomino na kirai kivumishi

Mfano: Mzee mwenye duka kubwa kule kijijini

             Watu wengi wenye matatizo ya kifedha

h.     IX.  Kiwakilishi pekee yake

Mfano: Wewe mimi yeye

i.        X.  Muundo wa  kiwakilishi na kivumishi

Mfano: Vyake vyake

              Wao wenyewe

II. KIRAI KIVUMISHI (KV)

Hiki ni kirai ambacho muundo wake umejikita katika kivumishi pamoja na neno au fungu la maneno linaloambatana na kivumishi.

N:B: Ingawa virai vivumishi hujibainisha kimuundo mara nyingi miuundo yake imekuwa ikichukuliwa kama sentensi kwa baadhi ya miundo ya virai nomino

Mfano: Watu wengi wana matatizo ya kifedha

                                                 KV

Mfano huu ni wa kirai nomino lakini ndani ya kirai nomino hicho kuna kirai kivumishi ambacho kimepigiwa mstari

MIUNDO YA VIRAI VIVUMISHI

a.      Kivumishi na kielezi chake

Mfano: baya sana

             Zuri sana

b.      Kivumishi  na kirai nomino

Mfano:      Enye duka kubwa

                  Enye nguvu nyingi

                  Enye macho makubwa

c.      Kivumishi na kirai kitenzi

Mfano:    enye kupenda fujo

d.      Kivumish na kirai kitenzi

Mfano:   Ingine – enye matatizo

e.      Kivumishi na kirai kiunganishi

Mfano: zuri wa kutamanisha

             Pungufu wa akili

 

III. KIRAI KITENZI

Hiki ni kirai ambacho muundo wake umekitwa katika mahusiano na kitenzi au uhusiano baina ya kitenzi na neno au fungu la maneno ambalo huambatana na kitenzi kimahusiano.

MIUNDO YA KIRAI KITENZI

a.    Kitenzi  peke yake

Mfano:  Anaringa

              Atapigwa

b.      Kitenzi na nomino

Mfano:  tumesemewa risala

                      KT

c.      Kitenzi na nomino mbili

Mfano: Tulimpa  mtoto chakula

                      KT

d.   Kitenzi na  kitenzi

Mfano:  Watoto wanaimba wakicheza

                        KT

e.      Kitenzi  nomino na kitenzi

Mfano:  tulimuomba mwalimu afundishe

                         KT

f.       Muundo wa ruwaza wa kitenzi “kuwa”

Mfano: a. Unaotokana na kitenzi na kivumishi

             –  Alikuwa mrefu

             b. Kitenzi na  kirai kiunganishi

             – alikuwa na pesa

             c. Kitenzi na nomino pahala (kielezi)

               – Alikuwa darasani

             d. Kitenzi kielezi na kitenzi

              -Itakuwa vizuri uwahi

IV. KIRAI KIELEZI (KE)

Tofauti na aina nyingine za virai miundo virai haijakitwa katika mahusiano baina ya neno kuu, yaani kielezi na neno au fungu la maneno linaloandamana na kelezi. Badala yake miundo ya kirai kielezi huwa inahusishwa maneno ambayo hufanya kazi kwa pamoja katika lugha kama misemo tu.

Mfano: Mara kwa mara

             -Mara nyingi

              -Sana sana

              -Haraka haraka

N:B     Dhima  kubwa  ya virai vielezi katika  sentensi ni kueleza jinsi, mahali wakati na sababu zilizofanya tendo Fulani lifanyike.

Tofauti na virai vingine  ambavyo nafasi yake ndani  ya sentensi huwa yakudumu, nafasi ya virai vielezi hubadilika yaweza kuwa mwanzoni au mwishoni mwa sentensi

Mfano: mwalimu alifundisha jana jioni

                                              KE

       Jana jioni mwalimu alifundisha

         KE

V.        KIRAI KIUNGANISHI

  Hiki ni kirai ambacho muundo wake umekitwa katika mahusinano baina ya maneno kama vile; kwa, na, katika, na kwenye katika fungu la maneno linaloambatana nacho. Kirai kiunganishini ni kirai ambacho neno kuu ni kiunganishi

NB: Katika lugha ya Kiswahili virai viunganishi vinamuundo mmoja tu nao ni ule wa kiunganishi na kirai nomino

Mfano: Kwa miguu

             Kwa amri ya jeshi

             Kwa baba yake

             Katika chumba

             Na mama

             Kwenye pombe

Japokuwa virai hivi vinamuundo mmoja, yaani kiunganishi na kirai nomino vinatofautiana sana kimaana.

Mfano: Baadhi ya virai viunganishi vinaonesha dhana ya uhusika naVingine vinadokeza dhana ya mahali au

a. Pahala; – Katika chumba

    Kwenye  pombe

    Kwa baba yake

b.Vingine vinadokeza dhana ya utumishi

Kama vile kwa kijiko

       Kwa miguu

C.Vingine hudokeza sababu – kwa amri ya jeshi

3.      KISHAZI

Hii ni tungo yenye kitenzi ambacho huweza kujitosheleza na kutoa taarifa iliyokamili au yaweza kuwa na kitenzi kisichojitosheleza na hivyo kushindwa kutoa taarifa iliyokamili au uliokusudiwa na mzungumzaji

Mfano: Msichana uliyemuona jana

             Msichana anasoma

              Mzee aliyepotea

              Mzee amepatikana leo asubuhi

AINA ZA VISHAZI

Kuna aina kuu mbili za vishazi

1.      KISHAZI HURU (k/Hr )

Kishazi huru ni kishazi kinachotawaliwa na kitenzi kikuu na hivyo  kukifanya kishazi hicho kutoa ujumbe unaojitokeza na kisichohitaji maelezo yoyote ya ziada

Mfano: Wanafunzi wanamsikiliza mwalimu

               -Mwalimu anafundisha wanafunzi

Vishazi hivi vinajitosheleza kwa sababu vinatoa ujumbe usiohitaji maelezo ya ziada

N:B: Vishazi vinahadhi sawa na sentensi sahili

II KISHAZI TEGEMEZI (K/TG)

Kishazi tegemezi ni kishazi ambacho kinatawaliwa na kitenzi ambacho hakikamilishi ujumbe ulokusudiwa na hivyo kukifanya kutegemea kitenzi kikuu cha kishazi huru ili kukamilisha ujumbe  ulikusudiwa na mzungumzaji.

Mfano:  –Wanafunzi waliokuwa darasani

              – Mwalimu aliyefundisha

Vishazi hivi ni tegemezi kwa sababu vinatoa ujumbe usiojitosheleza hivyo vinahitaji kuandamana  na kisha  huru  ili kukamilisha ujumbe uliokusudiwa.

Mfano : wanafunzi waliokuwa darasani wamefukuzwa shule.

              Mwalimu aliyefundisha amesimamishwa kazi.

N:B Kishazi tegemezi  hakikamilishi  ujumbe mpaka kiandamane na kishazi huru. Kishazi tegemezi kinapoambatana na kishazi huru vyote kwa pamoja hutengeneza sentensi changamano.

AINA  ZA VISHAZI TEGEMEZI

 

Vishazi tegemezi vinaweza kugawanya katika makundi makuu mawili

a.      Kishazi tegemezi kivumishi (K/TGV au BV)

b.      Kishazi tegemezi kielezi (K/TgE au BE)

KISHAZI TEGEMEZI KIVUMISHI

Vishazi tegemezi vumishi ni vishazi ambavyo huvumisha au hutoa maelezo zaidi kuhusu nomino zilizopo katika tungo, yaani nomino ya kiima au nomino ya shamirisho, kishazi tegemezi, kivumishi kinaweza kutokea kwenye kiima au kiima au kiarifu katika sentensi.

Mfano: Wanafunzi waliotoroka jana wanaadhibiwa leo asubuhi

                              BV

   Mwalimu amewaadhibu wanafunzi waliotoroka jana

                                                                     BV


KISHAZI TEGEMEZI KIELEZI

Hiki ni kishazi kinachotawaliwa na kitenzi ambacho huwa na utegemezi wa taarifa hiyo huhitaji kukamilisha taarifa hiyo kwa kuambatana na kitenzi kikuu cha kishazi huru. Kishazi tegemezi kielezi hutoa maelezo zaidi kuhusu kitezi kikuu kilichokuwepo katika tungo

Mfano:   Alikikata alipolima

BE

      Waalimu walipotuma   walitufukuza

                                       BE

Sifa za kishazi tegemezi

 Kishazi tegemezi kinasifa bainifu ambazo hukifanya kijulikane kiurahisi

i Hakiwezi kutoa maana kamili kama hakijaambatana na kishazi huru

 Mfano: Mwalimu alipoanza kufundisha

                                    B

                  Mzee uliyemuona jana

                                     B

ii. Kinaweza kuondolewa katika sentensi na  kisiharibu maana ya sentensi nzima

            Mfano:  Mbwa aliyepata kichaa ameuwawa

                            Watoto waliponiona walifurahi

 Kinaweza kutambulika kwa kuwepo vishazi vingine kama vile, ingawa, kwamba, ili, kwa sababu, au.

            Mfano:  -Mwalimu amesema kwamba wanafunzi wengi wamefaulu

                           – Wanafunzi ambao hawapo wataadhibiwa

                                                   B

                                 –   Ingawa walifika hatukuwaona

                                        B

                               –    Ili tuweze kuendeleza lazima tufanye kazi Kwa bidii

                                    B

 Kinaweza kutanguliwa au kikafuatwa na kishazi huru

      Mfano: nimemuona Rehema nilipokwenda

                       B

HADHI YA VISHAZI

Vishazi huru vinahadhi sawa na  sentensi sahili

Mfano: Ng’ombe  amechinjwa leo asubuhi

Kishazi tegemezi ambacho  huandamana  na kishazi huru,  hadhi yake hushuka  na hivyo  kukifanya kuwa na hadhi sawa na kirai /kikundi.

Mfano: Ng’ombe aliyenunuliwa jana
Hiki ni kishazi tegemezi na hadhi yake  imeshuka kulingan na kirai tena kira  nomino

 

DHIMA YA VISHAZI

Vishazi vinapotumika katika tungo huwa na dhima mbalimbali

 

–      Vishazi tegemezi vivumishi hufanya kazi kama vivumishi katika tungo.

Mfano: Mtoto asiyesikia amepotea

                               V

– Baadhi ya vishazi tegemezi hufanya kazi  kama vishazi

Mfano: Watoto wanaofurahisha wanavyoimba

                                             E

4.      SENTENSI

Sentensi ni kifungu cha maneno kinachoanzia neno moja na kuendelea lakini chenye muundo wa kiima na kiarifu au kikundi nomino na kikundi kitenzi

N.B;    Sentensi ndiyo tungo kubwa kuliko tungo nyingine zote katika mpangilio wa tungo

MUUNDO WA SENTENSI

Sentensi ina sehemu kuu mbili (2) Sentensi ikigawanywa kwa kutumia kigezo cha kidhima ina sehemu kuu mbili ambazo ni KIIMA na KIARIFU

Sentensi ikigawanywa kwa kuangalia muundo wa sentensi basi sentensi hugawanywa katika sehemu kuu mbili yaani KIKUNDI NOMINO na KIKUNDI KITENZI.

Mgawanyo huu hutokana na kanuni kuu ya kisintaksia ambayo hudai kila sentensi iliyosahihi  na inayokubaliwa na wazawa wa lugha ya Kiswahili ni lazima iwe na muundo wa kiima na kiarifu au kikundi nomino na kikundi kitenzi.

Kiima hutaja mtenda au mtendwa wa jambo na kiarifu huarifu jambo linalotendwa na kiima au alilotendwa na kiima

Mfano: Juma anacheza mpira.

Juma ni kiima yaani mtendwa  na kiarifu ni anacheza mpira

Hapa pia  nomino mpira ndiyo kiima, lakini kiima hiki kinataja kile kinachotendwa yaani mpira

        KIIMA

Kiima ni sehemu ya sentensi ambayo hujaza na nafasi ya mtenda au mtendwa katika sentensi

NB: aghalabu kiima hutokea upande wa kushoto wa kitenzi

Mfano:Mwalimu/anafundisha wanafunzi

                     K

              Wanafunzi/ wanafundishwa na walimu

                       K

Kwa kawaida kiima hukaliwa na jina au kikundi jina ambalo hujaza nafasi ya mtenda au mtendwa katika sentensi

VIPASHIO VYA KIIMA

Kiima kinajengwa na nini?

Kiima hujengwa na vipashio vifuatavyo

i.        Jina peke yake

Mfano: Mwalimu / anafundisha wanafunzi

                K

ii.     Jina na Jina

Mfano: Baba na mama/wanakula

                   K

iii.   Jina na kivumishi

Mfano: Mtoto mzuri/amepewa zawadi

                   K

iv.   Kivumishi na jina

Mfano: Yule mwizi/amekamatwa

                    K

v.      Kiswahili peke yake

Mfano: Wewe ni mzembe

                  K

vi.   Kiwakilishi na kivumishi

Mfano: Yule mzembe / amefukuzwa

                      K

vii.Kitenzi jina na jina

Mfano: Kulia kwa mtoto/kunasikitisha

                    K

viii.    Kitenzi jina na jina

Mfano: Kulia kwa mtoto/kunasikitisha

                        K

ix.   Kitenzi jina na  jina

Mfano: Kuungua kwa mtoto /kunasikitisha

                        K

x.     Kitenzi jina na kivumishi

Mfano: Kuimba na kucheza kwake/kunafurahisha

                           K

xi.   Jina  na kishazi tegemezi kivumishi

Mfano: Mtoto aliyepotea /amepatikana leo asubuhi

                           K

xii.Nomino, kivumishi na kishazi tegemezi kivumishi

Mfano: Mtoto mzuri uliyemuona jana/ni ndugu yangu

                               K

xiii.                     Kivumishi nomino kivumishi na Bv

Mfano, Yule mtoto uliyemuona jana /ni mwanafunzi

                                 K

      KIARIFU (A)

Hii ni sehemu muhimu zaidi katika sentensi na wakati mwingine huweza kusimama peke yake bila kiima kwa kuwa hubeba viwakilishi vya kiima. Kiarifu ni sehemu katika sentensi ambayo hukaliwa na maneno ambayo huarifu tendo lililofanywa, linalofanywa au litakalofanywa na kiima.

Mfano: Mwalimu/anafundisha wanafunzi darasani

                                                           A

VIPASHIO VYA KIARIFU

i.          Kitenzi kikuu peke yake

            Mfano: Mtoto anacheza

                           A

   ii.        Kitenzi kisaidizi au visaidizi vilivyo sambamba na  (T)kitenzi kikuu

   Mfano: Mtoto alikuwa anataka kucheza

                                             A

   iii.          Kitenzi kishirikishi na shamirisho

               Mfano: Watoto/wanacheza uwanjani

                                             A

     Iv        Kitenzi kikuu na chagizo

                 Mfano: Watoto/wanacheza uwanjani vizuri

                                                 A

       v.        Kitenzi kikuu shamirisho na chagizo

                   Mfano: Mwalimu/anafundisha wanafunzi darasani

                                                            A

vi.          Kitenzi kisaidizi kikuu na shamirisho

Mfano: Mwalimu /alikuwa anafundisha wanafunzi wengi

                                                A

vii.               Kitenzi kisaidizi kikuu na chagizo

Mfano: Mwalimu/alikuwa nafundisha darasani

                                                A

viii.                  Vitenzi visaidizi kikuu, shamirisho na chagizo

Mfano: Mzazi/alikuwa anataka kuwarudisha watoto wake nyumbani

                                                 A

        SHAMIRISHO (sh)

Shamirisho ni jina  au kikundi jina  (kirai nomino) kinachojaza nafasi ya mtendwa au mtenda, mtendwa katika sentensi. Shamirisho hutokea baada ya kitenzi kikuu au kitenzi kishirikishi katika sentensi,

 Shamirisho hujibu swali mtenda amemtenda nani, Au mtendwa ametendewa nini?.lakini pia mtendwa ametendwa na nani?

Mfano: Wanafunzi/wanasoma vitabu

                                                      Sh

                Juma/alimisomea Asha kitabu

                                                       Sh

        CHAGIZO  (ch)

Chagizo ni sehemu ya sentensi ambayo hutokea upande wa kiarifu ambayo huwa na neno au kikundi cha maneno ambacho hujaza nafasi ya kielezi.

Mfano:Mama /amekwenda nyumbani

                                                 Ch

  Mtoto /anacheza mpira vizuri sana

                                           Ch

N:B Chagizo huwezakutokea mara baada ya kitenzi kikuu au mara baada ya shamirisho

AINA  ZA SENTENSI

KKuna aina kuu nne za sentensi
Sentensi changamano
Sentensi  sahili/ huru.

3.      Sentensi shurutia
Sentensi Ambatano

1.SENTENSI SAHILI/HURU

Hii ni aina ya sentensi ambayo hutawaliwa na kishazi huru. Kishazi hicho kinaweza kuwa kifungu tenzi kimoja ambacho kinaweza kuwa na kitenzi kikuu au kitenzi kisaidizi na kitenzi kikuu au kitenzi kishirikishi na shamirisho

Mfano: Juma ni mzembe

             Juma alikuwa mzembe sana

             Mwalimu alikuwa nafundihsa darasani

 

MIUNDO YA SENTENSI HURU /SAHILI

Muundo wa kitenzi kikuu peke yake (tawaliwa)

Mfano: Wanacheza

             Alinipiga

             Wanasoma

i.Muundo wa kitenzi kikuu peke yake (tawaliwa)

Mfano: Wanacheza

             Alinipiga

             Wanasoma

ii.Muundo wa kitenzi na kitenzi kikuu

   Mfano: Alikuwa anasoma

               Walikuwa wanataka kufundishwa

ii Muundo wa kirai na kirai kitenzi

Mfano; Mwalimu anafundisha

             Wanafunzi wanamsikiliza

iii. Muundo wa virai vitenzi vilivyokitwa katika kitenzi kuwa

    Mfano: John alikuwa kijana mzuri

                  Mwalimu atakuwa darasani

                 Aisha angekuwa wa kwanza

V.Muundo ambapo virai nomino na virai kitenzi vinaambatana na vijalizo

Mfano: Baba yangu alinunua machungwa mawili usiku

SIFA ZA SENTENSI SAHILI/HURU

1.      .Inakiima ambacho kinaweza kutajwa wazi au kisitajwe kama kinaeleweka.

2.      Inakiungo ambacho kinaunda  kitenzi kikuu kimoja au kitenzi kiuu c akitenzi kisaidizi au kitenzi kuku na  shamrisha na chagizo

3.      Haifungamani na sentensi nyingine na inajitosheleza kimuundo na  kimaana

UCHANGANUZI WA SENTENSI SAHILI

Kuchanganua sentensi ni kitendo au mbinu ya kuitenga au kuigawa sentensi katika sehemu mbalimbali ambazo hujenga au kuiunda sentensi hiyo. Kuna mikabala mikuu miwili ya uchanganuzi wa sentensi,

1.      Kwa  kutumia mkabala wa kimapokeo ambapo sentensi hugawanywa  katika kiima na kiarifu na baadaye hufuatiwa na vipashio vinavyojenga  kiima na kiarifu

 

iii.        Mkabala wa kimuundo/ kisasa ambapo sentensi hugawanywa katika sehemu kuu mbili yaani kirai nomino na kirai kitenzi kisha hufuatwa na vipashio vijengavyo kirai nomino na kirai kitenzi

Mfano;    Wanafunzi wale walikua wanasoma darasani

 

N:B

Katika uchanganuzi wa sentensi ni muhimu kutofundishwa mikabala yote miwili (haipaswi)

Lakini kuna baadhi ya wataalamu wanachanganya mikabala yote Miwili katika uchanganuzi wao wa sentensi. Mfano; F.Nkwera (1978) TUMI (1988) J.S.Mdee (1996) Mohamed Taasisi ya dimu (1966)

UCHANGANUZI WAKE

i. Kutaja aina ya sentensi

ii Kutaja sehemu za sentensi yaani kiima/kikundi nomino, kiarifu/kikundi kitenzi

iii Kutaja vipashio vinavyojenga kiima na kiarifu

iv.Kutaja aina za maneno yote yaliyomo  katika sentensi

v.Kuandika upya sentensi hiyo.

AINA ZA UCHANGANUZI WA SENTENSI

Uchanganuzi wa sentensi hufuata

i.Mishale/ mistari

ii.Matawi/msonge/ngoe

iii.Maelezo/maneno

iv.Parandesi/mabano

v  jedwali/visanduku

1.      UCHANGANUZI WASENTENSI SAHILI

NJIA YA MANENO

A.MKABALA NA KIMPOKEO

                                i.     Mtoto Yule alikuwa anataka kucheza mpira wake uwanjani

Hii ni sentensi sahili

Kiima ni mtoto Yule

Kiima kinanomino na kivumishi

Nomino ni mtoto

Kivumishi ni  Yule

Kiarifu ni alikuwa anataka kucheza mpira wake uwanjani

Kiarifu kina vitenzi visaidizi viwili kitenzi kikuu, shamrisho, chagizo

Kitenzi kisaidizi cha kwanza ni alikuwa

Kitenzi kisaidizi  cha  pili  ni anataka

Kitenzi kikuu ni kuchezea

Shamirisho ni mpira wake

Nomino ni mpira

Kivumishi ni wake
Chagizo ni uwanjani
Kielezi ni uwanjani

B.MKABALA WA KISIASA

Mtoto  yule alikuwa  anataka  kuchezea mpira  wake uwanjani

Hii ni sentensi sahili

Kirai nomino ni “mtoto Yule”

Kirai nomino kina nomino  na kivumishi

Nomino ni  mtoto

Kivumishi ni Yule

Kirai kitenzi ni alikuwa anataka kucheza mpira  wake uwanjani

Kirai kitenzi kina vitenzi visaidizi  viwili kitenzi kikuu  kirai,nomino na kirai kielezi

Kitenzi kisaidizi cha kwanza ni alikuwa

Kitenzi kisaidizi  cha pili ni anataka

Kitenzi kikuu ni kucheza

Kirai nomino kina nomino na kivumishi

Nomino ni mpira
Kivumishi ni wake

Kirai kielezi  kina kielezi

Kielezi ni uwanjani

                             ii.            NJIA YA MISHALE

A.    MKABALA WA KIMAPOKEO

Mtoto Yule alikuwa anataka kucheza mpira wake uwanjani

B.     MKABALA WA KISASA

                                               III. NJIA YA MATAWI

IV. NJIA YA JEDWALI

A.    MKABALA  WA KIMAPOKEO

S.SAHILI
K                         A
                P       SH
                    N T N V
               JUMA NI MTOTO MWEMA

 

 

 

 

 

B.     MKABALA WA KISASA

 

S.SAHILI
KN             KT           
                P       KN
                    N T N V
               JUMA NI MTOTO MWEMA

 

 

 

 

 

2.SENTENSI CHANGAMANO

Ni sentensi inayotawaliwa na kishazi huru kimoja au zaidi, na kishazi tegemezi kimoja au zaidi. Kishazi huru/tegemezi hicho kinaweza kutokea upande wa kiima au kiarifu

Mfano:  Wanafunzi waliotoroka jana wameadhibiwa leo asubuhi

                                B

              Mwalimu amewaadhibu wanafunzi waliotoroka jana

                                                                     B

NB:     Sifa kubwa ya sentensi changamano ni kuwa na kishazi tegemezi ambacho hutegemea kishazi huru kilichomo ndani ya sentensi hiyo.

MIUNDO YA SENTENSI CHANGAMANO

Vishazi tegemezi vilivyomo ndani ya sentensi changamano ndiyo hutupatia miundo mbalimbali ya sentensi.

Hii ni miundo ambayo kirai nomino hubeba kishazi tegemezi kirejeshi ambacho hurejesha tendo kwa mtenda au mtendwa

Mfano: Mbuzi aliyenunuliwa juzi ameibwa leo asubuhi

                        BV

Miundo yenye vishazi tegemezi vielezi

Hii ni miundo ambayo vishazi tegemezi hurejelewa/hueleza hali ya vitenzi vilivyomo kutoka vishazi huru

Mfano: Mimi sikuvutiwa alivyosema

                                                BE

  Juma aliponiona alikimbia

                     BE

UCHANGANUZI WA SENTENSI CHANGAMANO

Uchanganuzi wa sentensi changamano huwa na hatua zifuatazo

i.Kutaja aina ya sentensi

ii.Kutaja kiima/kirai nomino na  kiarifu/kirai kitenzi

iii.Kutaja vishazi vilivyomo katika sentensi nakishakueleza kazi ya kila kishazi

Kwa mfano: Kutaja kama kishazi tegemezi kinavumisha jina au kikundi jina kilichopo katika kiini

                      Mfano: Mbuzi aliyenunuliwa juzi ameibwa leo asubuhi

                                         BV

                        Mwalimu aliwaadhibu wanafunzi waliotoroka

                                                                       Bv

b. Kutaja  kama kishazi  tegemezi kinavumisha  nomino au kikundi nomino kilichopo katika  shamirisho.

c. Kutaja kama kishazi tegemezi kinatoa maelezo zaidi kuhusu kitenzi kikuu kilichopo katika  kishazi huru

 Mfano: Juma aliponiona alikimbia

                      BE

Juma alikimbia aliponiona

                                               BE

Iv Kutaja aina zote za maneno katika sentensi hiyo

V.Kurudia kuandika sentensi hiyo

I. NJIA YA MATAWI.

A: MKABALA WA KIMAPOKEO

Mtoto aliyekuletea maji ya kunywa ni mwanangu

                                                       Mtoto   aliyekuletea      maji            ya             kunywa            ni      mwanangu

                              

SENTENSI SHURUTIA

Ni sentensi ambayo huwa na vishazi tegemezi viwili ambavyo utegemezi wake hutokana na mofimu “nge”- ngali –ngeli na –ki-. Mofimu hizi hufanya vishazi hivyo vitegemeane yaani kufanyika kwa tendo moja kunategemea tendo jingine au kutokuendeka kwa jambo fulani hutegemea kutokutendeka kwa jambo Fulani,

Mfano: Juma angejibu maswali yote angefaulu mtihani

            – Ukisoma kwa bidii utafaulu mtihani

N:B     Mofimu hizi zinapotumika  katika sentensi shurutia huwa hazitakiwi kuchanganywa

SWALI: Huku ukitumia mifano onesha tofauti iliyopo kati ya sentensi na tungo

NGELI ZA MAJINA (NOMINO)

Neno ngeli ni neno la Kiswahili lililotolewa kutoka lugha ya kihaya likiwa na maana ya vitu vinavyofanana au vinavyoshabihiana.

Kwa hiyo ngeli za nomino na makundi ya majina yanayofanana au yanayowiana kwa kutuma kigezo Fulani. Nomino za lugha ya Kiswahili zinaweza kuwekwa katika makundi yanayofananana kwa kutumia vigezo vikuu viwili.

i. )   Kwa kutumia kigezo cha mofolojia ya maneno hayo ambacho huyapanga majina  kwa kuangalia maumbo  ya umoja na wingi wa  majina hayo.

ii.) Ni kigezo cha kisintaksia ambacho huyagawa majina katika makundi yanayowiana kwa kuzingatia uhusiano uliopo   baina ya majina na vitenzi.Majina yote yanayohusiana kwa namna moja au kwa namna inayofanaa yanapoishia na vitenzi hufanya kundi moja la ngeli.

KIGEZO CHA KIMOFOLOJIA/MAUMBO YA UMOJA NA WINGI

Hiki ni kigezo kilichotumika na wanasarufi wa mwanzo ambao waliainisha majina kulingana na maumbo ya umoja na wingi au viambishi awali vya majina hayo. Majina hayo yanayofanana katika viambishi awali yaliwekwa katika kundi moja na kufanya kundi moja la ngeli. Kama sarufi hao wapo walioyagawa majina katika makundi kumi na nane(18) na uongozi ulioyagawa majina hayo katika  makundi tisa (9) lakini kwa kutumia kigezo hicho hicho cha  kimafolojia kwa kutumia  kigezo hiki tutayafafanua makundi  ngeli kumi na nane (18) za majina ya Kiswahili.

NGELI SIFA ZA MAJINA MFANO
1.Mu -Majina ya viumbe hai isipokuwa mimea m-tu wa –tu
2.Wa -Vitenzi jina vyote vinavyotaja watu vina m-toto wa- toto
-Vitenzi jina vyote vinavyotaja watu

Vinavyoanza na “m” katika moja na “wa” katika wingi

m-fungaji wa fugaji
3.M- -Majina  ya baadhi ya mimea m-ti     mi –ti
4Mi- -Majina ya vitu vyote vinavyoanza na “M” katika umoja na “mi”katika  wingi m-papai  mi – papai

m-pir mi-pira

M-sumeno mi-sumeno

-Majina ya matendo/vitenzi jina vinayoanza  na “m” katika umoja na “mi” katika umoja na “mi” katika wingi m-kasi mi-kasi

m-chezo mi- chezo

m-tupo mi-tupo

5.Ki
6 vi- -Majina  yote yanayoanza na “ki-“ katika  umoja na “vi-“ katika wingi Ki-nu    vi-nu

Ki-kapu  vi-kapu

Ki- umbe vi- umbe

-Majina  ya vitu vinayoanza  na “ch” katika  umoja na “vy”  katika wingi ki-goda    vi-goda

ch-akula vy-akula

ch-uma  vy-uma

-Majina ya viumbe yanayoambikwa kiambishi”ki” mwanzoni  cha kuvumisha Ki-zee   vi-zee

Ki-vulana  vi-vulana

Ki-toto  vi-toto

7.Ji- -yanaingia  majina yanayoanza na
8.Ma Ji-katika umoja na wingi Ji-cho     ma –we
-Majina  ya baadhi ya sehemu sa mwili wa binadamu wanyama au sehemu za mtu Ji – cho     ma-cho

Goti         ma-goti

Ji-no        meno

-Majina ya mkopo yenye kuanzana “ma” katika wingi Sikio       ma-sikio

Maziwa   maziwa

-Majina yenye kueleza dhana ya wingi japokuwa hayahesabiki Shati        ma-shati

Bwana     ma – bwana

Ua      ma – ua

-Majina yote yanayoanzia na N-na kufuatwa na konsonati ch, d, g, j, z, y katika umoja na wingi Njaa,nguo, nchi, ndoa nzi

Nje, nyumba

9           N -Majina yanayoanza na M- na Mb Mbuga, mboga, mvua mvinyo, mvi, mbao,  taa
10 -Majina  ya mkopo
N:B: Maumbo ya umoja na wingi katika  majina  haya haya badiliki Kalamu
11U

12N

-Majina  yote yanayoanza na

U- katika umoja  na N-au

Mb- katika wingi

U-so   N-nyuso

U-zi      N-yuzi

U – bao  Mb – ao

u-limi   ndimi

13 U -Majina yote  yanayoanza na U-asi    ma – asi
14Ma U – katika umoja -ma-

Katika wingi

U-gonjwa   ma – gonjwa

U-gonjwa  ma-gonjwa

15 ku Majina  yanayotokana na vitenzi vinavyoonea ku- mwanzoni Ku – imba

Ku –cheza

Ku-la

16. Pa Huonesha mahali pa mbali

Kidogo palipo wazi

 pahala
17. Mu Kuonesha mahali pa mbali lakini ndani Mule
18.ku Mahali pa mbali zaidi kule

FAIDA ZA UAINISHAJI  NGELI KIMOFOLOJIA

1.      Hutumika kuonesha uhusiano wa lugha zenye  asili moja

Mfano: Lugha ya Kiswahili na lugha mbalimbali za kibantu. Majina mengi ya lugha ya Kiswahili yana maumbo dhahiri ya umoja na wingi pia majina mbalimbali ya lugha za kibantu yana sifa hiyo.

2.      Ni rahisi kugawanya majina hasa yale yenye maumbo ya umoja na wingi katika makundi mbali mbali kwa kutumia kigezo hiki.

3.      Kutumika kuonesha maumbo  ya umoja na wingi katika nomino

MATATIZO YA  UAINISHAJI KIMOFOLOJIA

1.  –   Ni vigumu kuyapanga majina yasiyokuwa na maumbo ya umoja na wingi katika makundi yake kwa kutumia vigezo hiki.

2.  – Hakitilii maanani miundo ya sentensi kwa mfano nomino kama kipofu, kiongozi, kijana, zilipaswa kuwa katika ngeli ya ki-vi lakini zimepelekewa katika ngeli ya kwanza kwa kuwa zinaoana kimuundo na nomino nyingine za kundi hilo. Nomino hizo kimefolojia zinatofautiana na nomino nyingine za ngeli ya kwanza na ya pili.

3.    –  Hakikidhi mahitaji ya sulubu na sentensi .

Mfano: Kitabu changu kimepotea

            Vitabu vingi vimepotea

            Kisu changu kimepotea

            Visu vyangu vimepotea

            Kijana wangu amepotea

            Vijana wangu wamepotea

Baadhi ya  nomino hazikidhi sababu za sentensi

4.   Kuna viambishi vya ngeli vinavyofanana na kujirudia rudia  kwa baadhi ya makundi ya majina. Mfano kiambishi mu – kinajitokeza katika ngeli ya  makundi ya majina. Mfano kiambishi  mu – kinajitokeza  katika ngeli  3; ngeli  kiwakilishi  ma-cha ngeli ya 8;  kinajitokeza katika ngeli  ya 1

Kiambishi N. Kinajitokeza katika  ngeli ya kumi na mbili pia kinatumika katika ngeli  ya tisa na ya kumi.

KIGEZO CH A KISINTAKSIA

Hiki ni kigezo ambacho huyagawa majina katika makundi mbalimbali kutokana na kigezo cha upatanisho wa kisarufi uliopo kati ya maji na viambishi awali vilivyopo katika vitenzi ambavyo huyapatanisha majina hayo na vitenzi.

Majina yote yanayotumia viambishi awali vipatanishi vinavyofanana huwekwa katika kundi moja na kufanya kundi moja la ngeli. Kwa  kutumia kigezo hiki kuna jumla ya  ngeli tisa za nomino

NGELI Viambishi awali vipatanishi Mfano
a -wa a -wa Kiongozi amepotea/viongozi wamepata
 a-umoja, Simba  amepotea/simba wamepotea
 wa-wingi
u-i u-(umoja) Mto umefunika
i-(wingi) Mito imefunika
Mti umeanguka
Miti imeanguka
Li – ya li-(umoja) Yai limevunjika
Ya-(wingi) Mayai yamevunjika
Gari limetengenezwa
Magari yamebaribika
Ki-vi Ki – (umoja) Kiti kimevunjika
Vi-(wingi) Viti vimevunjika
Chakula  kimemwagika
Vyakula vimemwagika
i-zi i-(umoja) Nchi imefilisika
Zi-(wingi) Nchi zimefilisika
u-zi u-(umoja) Ukuta umebomoka
Zi(wingi) Kuta zimebomoka
Ubao umechafuka
Mbao zimechafuka
u-ya u-(wingi) Ugonjwa umeenea
Ya-(wingi) Magonjwa  yameenea
Ubaya umeongezeka
Mabaya yameongezeka
ku Ku- Kucheza kunafurahisha
Kula kwake kunasikitisha
Kuimba kwao kunapendeza
Pa Pale panapendeza
Mu Mule mwanagiea
Ku Kule kunapendeza

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

FAIDA ZA KIGEZO HIKI

1.  –    Hutumika kama kigezo cha  ulinganifu wa lugha haswa Kiswahili na lugha za kibantu

2.    –  Hutumika kuyapanga majina katika makundi yanayofanana

3.      -Huweza kuyaweka majina katika makundi  kiurahisi zaidi hata yake yasiyokuwa na maumbo ya umoja na wengi ilimradi yahusiane kisarufi

 

MATATIZO YA KIGEZO HIKI

1.      Katika ngeli ya kwanza kuna vipatanishi viwili vya umoja ambavyo ni yu na-a- kiambishi yu – ni cha Kiswahili cha kilahaja sio Kiswahili sanifu.

2.      Huyaweka majina yenye maumbo na sifa tofauti katika kundi moja. Mfano nomino za kipekee kama vile Juma Amina Latifa na zile za kawaida kama vile chura, kaka  ,mama , baba

3.      Kuna baadhi ya majina ambayo viambishi vipatanishi vina utata hivyo inakuwa vigumu kuyainisha mfano: Jambazi amepigwa risasi /majambazi yamepigwa risasi

4.      Kuna vipatanishi vinavyofanana katika ngeli.Mfano kiambishi -u- cha umoja katika ngeli ya pili kinajitokeza katika ngeli ya sita na ngeli ya saba. Kiambishi kipatanishi i – cha wingi cha ngeli ya pili kinajitokeza katika ngeli ya tano umoja na kiambishi patanishi “zi” wingi cha ngeli ya tano kinajitokeza katika ngeli ya sita wingi

MATUMIZI  YA NGELI

1.      Hutumika kuyapanga majina katika makundi yanayoshabihiana kwa kutumia kigezo maalumu mfano: kimofolojia  na kisintaksia

2.      Hutumika kutambulisha maumbo ya umoja na wingi katika nomino na vivumishi. Mfano;

M-toto, m-zuri

Ki-tabu ki-zuri

3.      Hutumika kuonesha upatanishi wa  kisarufi   uliopo kati nomino, vivumishi na vitenzi mfano: Mtoto mzuri amepata

                   -Kitu kizuri kimepotea

4.      Hutumika kuonesha uhusiano baina ya lugha ya Kiswahili lugha mbalimbali  za kibantu

MATUMIZI YA SARUFI

MADA ZOTE ZA KISWAHILI KIDATO CHA TANO BOFYA HAPO CHINI KWA KILA KUSOMA MAADA

FASIHI KWA UJUMLA 

MAENDELEO YA FASIHI SIMULIZI

MAENDELEO YA KISWAHILI

MATUMIZI YA SARUFI

UTUNGAJI

UTUMIZI WA LUGHA

 

ALSO READ

O, LEVEL FULL STUDY NOTES FOR ALL SUBJECTS

A’ LEVEL FULL STUDY NOTES FOR ALL SUBJECTS

 

 

1 thought on “KISWAHILI KIDATO CHA TANO:MATUMIZI YA SARUFI”

Leave a comment