SERIKALI YAMWAGA AJIRA KWA WAALIMU SHULE ZA MISINGI NA SEKONDARI

Posted on

SERIKALI YAMWAGA AJIRA KWA WALIMU SHULE ZA MISINGI NA SEKONDARI

SERIKALI YAMWAGA AJIRA KWA WALIMU SHURE ZA MISINGI NA SEKONDARI

USIBAKI NYUMA>PATA NOTES ZETU KWA HARAKA:INSTALL APP YETU-BOFYA HAPA

 

UNAWEZA JIPATIA NOTES ZETU KWA KUCHANGIA KIASI KIDOGO KABISA:PIGA SIMU:0787237719

 

FOR MORE NOTES,BOOKS,SCHEMES OF WORKS,PAST PAPERS AND ANALYSIS CLICK HERE

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema Serikali inaendelea na taratibu za kuajiri walimu 12,000 wapya kwa Shule za Msingi na Sekondari na zitakapokamilika zitatangazwa.

Ameyasema hayo  alipokuwa akizungumza kwenye siku ya TAMISEMI ya kueleza mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka mitano katika sekta ya elimu iliyofanyika katika ukumbi wa  shule ya Sekondari Dodoma.

Amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitano walimu zaidi ya 18,000 wameajiriwa na kupelekwa Shule za Msingi na Sekondari na kwamba ajira zingine 12,000 zilizoelekezwa na Rais John Magufuli bado taratibu zake zinaendelea.

“Nafahamu bado kuna changamoto ndio maana Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli  ametoa maelekezo ya kuongeza ajira za walimu  na ametoa maelekezo ya ajira zaidi ya 12,000 taratibu zinaendelea zikikamilika Serikali itaongeza  ajira zingine kwa shule za msingi na sekondari,”amesema Mhe. Jafo.

Akizungumzia kuhusu mafanikio yaliyopatikana kwa miaka mitano katika Sekta ya Elimu ya Msingi na Sekondari Mhe.Jafo amesema katika kipindi hicho kiasi cha Sh.Trilioni 1.09 zimetolewa kwa ajili ya elimu bila malipo.

Amefafanua kuwa  kuwa zaidi ya Sh.Bilioni 502 zimetolewa kwa ajili ya elimu ya Shule za Msingi na Sh.Bilioni 593.9 zimeenda sekondari, jambo ambalo limesaidia watoto wa maskini kupata elimu.

“Mwaka 2016 watoto wengi walifurika kwenye shule zetu wakati zikiwa zimekadiria watoto 200 hadi 400, zingine ziliweza kusajili hadi wanafunzi 1,000, kwa mfano shule ya Nyakanazi na Majimatitu na watoto wengine walisajiliwa wakiwa na miaka 10 kutokana na miaka mitatu nyuma walikosa fursa hiyo,”amesema Jafo.

Ameendelea kufafanua kuwa  katika kipindi cha miaka mitano zaidi ya Sh.Bilioni 501 zimetolewa kwa ajili ya kuboresha miundombinu mbalimbali na hadi kufikia mwezi Juni 2020 ujenzi wa shule mpya za Msingi 905 zilikuwa zimekamilika hivyo  kuongeza idadi ya shule za Msingi kutoka 16,899 mwaka 2015 hadi 17,804 mwaka 2020.

Pia amesema  vyumba vya madarasa 17,215 vimejengwa na kuongezeka kutoka vyumba 108,504 mwaka 2016 hadi 125,719 mwaka 2020, sawa na ongezeko la asilimia 13.7 ambapo ujenzi wa vyumba 3,049 unaendelea na ukikamilika idadi ya vyumba vya madarasa kwa shule za Msingi itafikia 128,768.

Aidha, amesema serikali imejenga shule mpya za Sekondari 228 na hivyo kuongezeka kutoka shule 4,708 mwaka 2016 hadi 5,330 mwaka 2020.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mhandisi Joseph Nyamhanga, amesema uwekezaji na maboresho yaliyofanyika katika sekta ya elimu kwa shule za msingi na sekondari umesaidia kuongeza kiwango cha ufaulu katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kutoka asilimia 67.84 mwaka 2015 hadi asilimia 81.50 mwaka 2019.

Naye, Naibu Katibu Mkuu, Tamisemi anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli, amesema  Mpango wa Elimu bila malipo ulianzishwa mahsusi baada ya utafiti walioufanya mwaka 2014 kuonyesha kuwa Watoto milioni 3.5 wapo nje ya Shule kutokana na kukosa ada.

Dear our readers and users you can also navigate our all study notes in our site

though this post please to read our notes by classes click lick button down

form one notes form two notes

form three notes form four notes

 

 

JE UNAMILIKI SHULE AU BIASHARA NA UNGEPENDA IWAFIKIE WALIO WENGI?BASI TUNAKUPA FURSA YA KUJITANGAZA NASI KWA BEI NAFUU KABISA BOFYA HAPA KUJUA

 

But for more post and free books from our site please make sure you subscribe to our site and if you need a copy of our notes as how it is in our site contact us any time we sell them in low cost in form of PDF or WORD.

 

 

UNAWEZA JIPATIA NOTES ZETU KWA KUCHANGIA KIASI KIDOGO KABISA:PIGA SIMU:0787237719

 

SHARE THIS POST WITH FRIEND

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *