Wanafunzi kumi bora kitaifa matokeo darasa la Saba 2020
Nafasi kitaifa | Jina la mwanafunzi | Shule ya msingi aliyotoka | Mkoa |
1 | Herrieth Japhet Josephat | Graiyaki | Mara |
2 | Huma Masala Huma | Kwema Morden | Shinyanga |
3 | Gregory Mtete Alphonce | Twibhoki | Mara |
4 | Nyambina Musa Nyambina | Graiyaki | Mara |
5 | Andrew Elias Mabula | Kwema Morden | Shinganya |
6 | Jonas Nyamataga Ayubu | Little Flower | Mara |
7 | Emmanuel Kashinje Paul | Kwema Morden | Shinganya |
8 | Emmanuel Peter Marwa | Kwema Morden | Shinganya |
9 | Prosper Aspenas Tumbo | God’s Bridge | Mbeya |
10 | Yesaya Mnkondo Bendera | God’s Bridge | Mbeya |
BOFYA HAPA KUTAZAMA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2020
Wanafunzi kumi bora kitaifa
Watahiniwa bora kitaifa wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi ni wale ambao wamepata alama nyingi zaidi kuliko wenzao kwenye masomo matano waliyotahiniwa.
Baraza la Mitihani la Taifa nchini Tanzania (Necta), limemtaja mwanafunzi aliyehitimu shule ya msingi Graiyaki iliyopo mkoani Mara, Herrieth Japhet Josephat kuwa ndiye aliyeibuka kinara katika matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi (Psle).
Herrieth anakuwa msichana pekee kati ya watahiniwa 10 bora kitaifa, waliotajwa na baraza leo Jumamosi, Novemba 21, 2020 wakati Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde akitoa taarifa ya matokeo hayo.
“Watahiniwa hawa bora kitaifa ni wale ambao wamepata alama nyingi zaidi kuliko wenzao kwenye masomo matano waliyotahiniwa, ambapo pia kuna mchanganuo kwa wasichana 10 bora, wavulana 10 bora,” alisema Dk Msonde.
Alimtaja aliyeshika nafasi ya pili kuwa ni Huma Masala Huma kutoka shule ya msingi Kwema Morden ya Shinyanga na nafasi ya tatu ikienda kwa Gregory Mtete Alphonce kutoka Twibhoki shule ya msingi iliyopo mkoani Mara.
Aliyeshika nafasi ya nne ni Nyambina Musa Nyambina kutoka shule ya msingi Graiyaki iliyopo Mara pia.
TAZAMA VIDEO
Chanzo cha msingi-Mwananchi